Sports

Swaleh Afungiwa Kushiriki Michezo Yoyote Kwa Tuhuma Za Ulawiti Mombasa

Published

on

Shirikisho la soka nchini FKF tawi la Mombasa limemsimamisha kwamda kocha wa vijana M’barak Swaleh katika shughuli zote za soka kufuatia madai unajisi yanayomuandama.

Swaleh anatuhumiwa kwa kosa la kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 12 madai anayodaiwa kuyatekeleza kati ya Januari na Agosti 14, 2025, katika eneo la uwanja wa soka wa Fort Jesus, eneo bunge la Mvita.

Katibu mkuu wa FKF Mombasa, Stephen Murithi, amesema kuwa shirikisho hilo linafuata misingi ya sheria na halitavumilia aina yoyote ya ukatili au unyanyasaji wa kijinsia ndani ya mchezo wa soka.

Aidha, Murithi ametoa onyo kali kwa makocha wote na wadau wa soka watakaopatikana wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji, akisema kuwa hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayepatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version