Sports
Swaleh Afungiwa Kushiriki Michezo Yoyote Kwa Tuhuma Za Ulawiti Mombasa
Shirikisho la soka nchini FKF tawi la Mombasa limemsimamisha kwamda kocha wa vijana M’barak Swaleh katika shughuli zote za soka kufuatia madai unajisi yanayomuandama.
Swaleh anatuhumiwa kwa kosa la kumnajisi mtoto wa umri wa miaka 12 madai anayodaiwa kuyatekeleza kati ya Januari na Agosti 14, 2025, katika eneo la uwanja wa soka wa Fort Jesus, eneo bunge la Mvita.
Katibu mkuu wa FKF Mombasa, Stephen Murithi, amesema kuwa shirikisho hilo linafuata misingi ya sheria na halitavumilia aina yoyote ya ukatili au unyanyasaji wa kijinsia ndani ya mchezo wa soka.
Aidha, Murithi ametoa onyo kali kwa makocha wote na wadau wa soka watakaopatikana wakijihusisha na vitendo vya unyanyasaji, akisema kuwa hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakayepatikana.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

