Sports
Vipusa wa Kenya waiparuza Ethiopia na kufuzu kwa raundi ya tatu
Timu ya taifa ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 Rising Starlets imefuzu kwa raundi ya tatu ya mechi za kuwania tiketi kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kuinyuka Ethiopia mabao 4-0.
Mechi hiyo ya marudio ya raundi ya pili iliyopigwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Ulinzi ilishuhudia Elizabeth Mideva, akipachika mabao mawili huku Valerie Nekesa na Fasila Adhiambo wakiongeza moja kila moja.
Kenya imefuzu kwa raundi ya tatu itakapochuana na Tanzania Februari mwaka ujao kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya mkumbo wa kwanza kumalizikia sare ya bao 1 wiki jana mjini Adis Ababa.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

