Connect with us

Sports

Wachezaji wa akiba wa Arsenal, walifunga na kuipa Kilabu hiyo Ushindi wa kwanza ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne.

Published

on

Kilabu ya Arsenal ambao walifika hatua ya nusu fainali msimu uliopita walianza kwa ushindi nchini Basque baada ya kutamba katika mchezo wa ushindani uliofanyika kwenye uwanja wa San Mames, ikiwa ni mechi ya kwanza kati ya nane za makundi.

Kikosi cha Mikel Arteta, ambacho kinawinda kombe hilo kubwa la kwanza tangu 2020 na ushindi wao wa kwanza kabisa kwenye Ligi ya Mabingwa, kilipata ushindi huo kwa ulinzi thabiti na mabao ya dakika za mwishoni. Martinelli alifunga dakika ya 72, sekunde 36 tu baada ya kuingia uwanjani, kabla ya Trossard kuongeza la pili dakika ya 87, huku kila mmoja akimsaidia mwenzake.

Athletic, waliorejea kwenye mashindano haya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 11, walikuwa bora mwanzoni wakiwa na sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa nyumbani.

Kocha wao Ernesto Valverde aliwapanga wachezaji wote waliokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa, akiwemo mshambuliaji tegemeo Inaki Williams lakini bila kaka yake Nico Williams aliyekuwa majeruhi.

Arsenal walianza na Wahispania wanne, wakiwemo viungo wawili wa Basque, Mikel Merino na Martin Zubimendi, ambao zamani walichezea wapinzani wa Athletic, Real Sociedad.

The Gunners, waliokuwa bila wachezaji muhimu akiwemo Bukayo Saka, walianza kubadilisha mchezo kupitia harakati za Viktor Gyokeres na msisitizo wa Noni Madueke upande wa kulia.

Mshambuliaji wa Kiswidi Gyokeres alipata shuti lililookolewa na Unai Simon, kisha akapiga kichwa kilichopita pembeni baada ya kufikia krosi ya hatari ya Jurrien Timber.

Alejandro Berenguer alipiga shuti lililopita lango kwa nafasi ya kwanza ya Athletic kabla ya mapumziko.

Gyokeres, akiwa na bandeji baada ya kuumia kichwani na kuvuja damu, alipiga kichwa nje akimalizia mpira wa adhabu wa Declan Rice.

Williams alizuiwa na David Raya huku Merino akikosa nafasi nyingine alipopiga kichwa moja kwa moja kwa Simon, mechi ikionekana kuongezeka kasi.

Arteta alimtoa Eberechi Eze aliyekuwa hafanyi vizuri na kumwingiza Martinelli, na mara moja akapata bao alilokuwa akilitafuta baada ya Arsenal kushambulia kwa kasi.

Martinelli alikimbia akiunganisha pasi ya Trossard, akagusa mpira vizuri kumwacha Andoni Gorosabel nyuma kisha akafyatua chini ya Simon.

Mbrazil huyo alihusiana pia na bao la pili, alipopeleka krosi nyuma kwa Trossard, ambaye alifunga kwa msaada wa mguso uliompoteza Simon.

Arsenal walijiimarisha sana majira ya kiangazi kuongeza wingi wa kikosi chao, hasa safu ya ushambuliaji, na faida yake ikaonekana hapa.

Arteta pia aliwapa nafasi ya kwanza wachezaji wapya Christian Norgaard na Piero Hincapie mwishoni mwa mchezo.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Sports

Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting

Published

on

By

Mshambuliaji Kai Havertz aliifungia Arsenal F.C. bao la ushindi katika dakika za mwisho kabisa, na kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Sporting CP katika mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya UEFA Champions League iliyochezwa Jana usiku.

Kikosi cha kocha Mikel Arteta kilifika katika Uwanja wa Estadio Jose Alvalade kikiwa kimeathiriwa na vipigo viwili mfululizo dhidi ya Manchester City F.C. kwenye fainali ya Kombe la Ligi na Southampton F.C. katika robo fainali ya Kombe la FA.

Kwa mara nyingine, Arsenal haikucheza kwa kiwango chake bora, lakini ilifanikiwa kupata ushindi kutokana na uokoaji mzuri wa kipa David Raya pamoja na umakini wa Havertz aliyefunga bao la ushindi katika muda wa nyongeza.

Arsenal sasa ina nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali kabla ya mechi ya marudiano itakayochezwa kaskazini mwa London tarehe 15 Aprili, ingawa italazimika kuboresha kiwango chake ikiwa inataka kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza.

Vipigo dhidi ya City na Southampton vilikuwa mara ya kwanza msimu huu kwa Arsenal kupoteza mechi mbili mfululizo, huku kipigo cha Kombe la FA kikiwa cha tano kwao msimu huu.

Athari za matokeo hayo bado zilionekana Lisbon, ambapo Arsenal ilipata ugumu wa kucheza kwa mwendelezo mzuri, lakini kama ilivyokuwa mara kadhaa msimu huu, walipata njia ya kushinda licha ya kutocheza vizuri.

katika mechi nyingine hatua ya robo fainali ni kwamba Bayern Munich waliondoka na ushindi wa magoli 2-1 mikononi mwa Real Madrid katika uwanja wao wa nyumbani Estadio Santiago Bernabeu.

Magoli ya Bayern yakitiwa kimyani na mshmabulizi Luis kipindi cha kwanza naye Erling Haaland kipindi cha pili.

Mechi ya marudiano itachezwa juma lijalo April 15.

Continue Reading

Sports

Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)

Published

on

By

Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.

Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.

SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

Continue Reading

Trending