Sports
Wakenya Kipyegon na Chebet kutimka nusu fainali ya mita 5,000 leo Tokyo
Mabingwa wa Dunia katika mbio za mita 10,000 Beatrice Chebet na Faith Kipyegon wa mita 1,500, watakutana leo kwenye nusu fainali ya mita 5,000, huku mashindano ya Riadha Duniani yakiingia siku ya sita mjini Tokyo, Japan.
Chebet ambaye pia ni bingwa wa Olimpiki katika mbio hizo za mizunguko 12 unusu atashiriki mchujo wa kwanza kuanzia saa saba adhuhuri pamoja na Margaret Akidor anayeshiriki mashindano ya Dunia kwa mara ya kwanza.
Kipyegon ambaye alishinda taji ya nne ya Dunia katika mita 1,500 atashiriki mchujo wa pili pamoja na mshikilizi wa rekodi ya Dunia ya kilomita 10 Agnes Jebet Ngétich aliyemaliza wa nne katika fainali ya mita 10,000.
Mrusha Sagai Julius Yego ataingia uwanjani saa 1.23pm kusaka nishani katika fainali za Urushaji Sagai.
Kenya ni ya pili kwenye msimamo wa medali kwa dhahabu 4, fedha 1 na shaba 2, nyuma ya Marekani yenye dhahabu 7, fedha 1 na shaba 2.
Makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yatakamilika Jumapili hii Septemba 21.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

