Sports
Wakenya Timothy na Reynold Cheruiyot wafuzu kwa fainali ya mita 1500, Tokyo
Bingwa wa Dunia wa mita 1500 mwaka 2019 Timothy Cheruiyot na bingwa wa dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 Reynold Cheruiyot wamejikatia tiketi kwa fainali ya mashindano ya Riadha Uimwenguni jijini Tokyo, Japani.
Cheruiyot alifuzu kwa fainali baada ya kumaliza wa nne katika nusu fainali ya kwanza leo Jumatatu akitimka kwa muda wa dakika 3 sekunde 35 .61.
Upande wake, Reynold aliongoza mchujo wa pili kwa muda wa dakika 3 sekunde 36.64 na kufuzu kwa fainali ya Jumatano.
Mkenya mwingine, Wiseman Were alifuzu kwa nusu fainali ya mita 400 kuruka viunzi.
mbio hizo zinaingia siku ya nne mjini Tokyo Japan .
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

