Sports
Diani Stars na Mwanambeyu Girls washinda mashindano ya kwanza ya soka ya ufukweni ya FKF Kaunti ya Kwale
Kilabu ya Diani Stars walitwaa ubingwa wa wanaume baada ya kuichapa Barbados 4-2, huku Mwanambeyu Girls wakinyakua taji la wanawake kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Diani Queens.
Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Hussein Mohammed, alisema shirikisho litaendelea kuunga mkono kandanda ya mashinani ili kukuza vipaji zaidi miongoni mwa vijana. Aliongeza kuwa watawekeza kwenye soka ya ufukweni ili kukuza utalii wa michezo, huku akiwataka wawekezaji zaidi kuungana na kushirikiana katika kuandaa mashindano mengi zaidi.
Mashindano hayo, ambayo yalianza mwezi Mei yakichezewa ufukwe wa Kongo mjini Diani, yalihusisha jumla ya timu 24 — timu 16 za wanaume na 8 za wanawake.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

