Sports
Faith Kipyegon Akosa Rekodi Kwa Sekundi 06.42
Mkenya na bingwa mara tatu wa mbio za Olimpiki mita 1500 Faith Kipngetich Kipyegon akosa kuvunja rekodi na kukimbia maili moja chini ya dakika 4 baada ya kukosa kwa muda wa sekunde 06.42 ugani Stade Charlety Ufaransa.
Mwanariadha huyo nguli alirejea jana Paris mji ambao mwaka 2023 alivunja rekodi yake mwenyewe kwa kutumia muda wake bora dakika 4.07.64 katika mji wa Monaco.
Hapo jana kwa usaidizi wa viatu maalum na wasaidizi uwanjani stade charlety Kipyegon alikua anaandikisha rekodi kwa kuwa mwanamke wa kwanza kukimbia mile moja chini ya dakika 4 ila lengo lake halikutimia huku akikosa milioni 13 ambayo ilikua imetolewa na wadhamini wa mchezo huo duniani.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

