Sports
Isak Na Newcastle United Sasa Njia Panda
Mshambulizi wa timu ya taifa ya Uswidi, Alexander Isak, ameieleza klabu ya Newcastle United kuwa hatacheza tena kwao katika taaluma yake ya soka.
Isak ameeleza wazi kuwa yuko tayari kutafuta timu mpya nje ya Uwanja wa St. James’ Park, licha ya The Magpies kusisitiza kwamba hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo.
Klabu ya Liverpool imeonyesha nia ya kumsajili Isak, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 25 kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Newcastle mwaka 2023 akitokea Real Sociedad kwa ada ya pauni milioni 70, na tangu wakati huo amecheza michezo 86 na kufunga mabao 54.
Newcastle wamesema wako tayari kumwachia mchezaji huyo endapo tu watampata mbadala wake, huku wakitaka zaidi ya pauni milioni 150 ili kumruhusu kuondoka.
Liverpool wako tayari kutoa pauni milioni 120 kwa Isak, wakilenga kuimarisha safu yao ya ushambuliaji baada ya kuondoka kwa Darwin Núñez, aliyejiunga na Al Hilal.