Connect with us

Business

Lishe Bora Yaongeza Uzalishaji wa Maziwa Kilifi, Lakini Soko Labanwa

Published

on

Wafugaji ng’ombe za maziwa kaunti ya Kilifi wamesema kiwango cha maziwa wanachopata kwa sasa kimeongezeka msimu huu wa mvua ikilinganishwa na msimu wa kiangazi.

Kulingana ma mmoja wa wafugaji hao katika kijiji cha Bodoi Wadi ya Junju kaunti ya Kilifi Leonard Zuma,kwa sasa wanapata maziwa mengi ikilinganishwa na miezi ya nyuma kutokana na upatikanaji wa urahisi wa nyasi.

Akizungumza na meza yetu ya Biashara ,Zuma amesema kwamba kwa sasa anatoa lita 20 kwa kila ng’ombe kinyume na hapo awali.

“ kwa sasa nyasi zinapatika kwa wingi ikilinganishwa na hapo awali ambapo tulikuwa tunanunua nyasi jambo ambalo limefanya kiwango cha maziwa kuongezeka.”

Hata hivyo Zuma amedokeza kuwa hakuna soko la kupeleka maziwa yao hali ambayo inapelekea kwamba kwa sasa wanapitia changamoto ya uhaba wa wateja katika soko la maziwa kutokana na hali ya uchumi ilivyo kwa sasa huku akilalamika ughali wa daktari wa ng’ombe.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

Bei za mafuta kuongezeka katikati ya mwezi aprili

Published

on

By

Kenya sasa inakabiliwa na hatari ya kupanda kwa bei za mafuta, huku mgogoro unaoendelea mashariki ya Kati ukianza kuathiri bei nchini.

Serikali sasa imeonya kuwa kufikia katikati ya mwezi Aprili, bei za mafuta huenda zikapanda ikionya kuwa ongezeko la bei ya mafuta kwa sasa haliwezi kuepukika kufuatia kupanda kwa bei za mafuta kimataifa.

Waziri wa hazina kuu ya kitaifa John Mbadi aliwahakikishia wakenya kuwa hakuna cha kuhofia kwani wameweka mikakati kupunguza athari zake.

Ili kupunguza athari za bei za mafuta kuongezeka, serikali ilisema itatumia shilingi bilioni 17 kutoka mfuko wa ada ya uwekezaji wa mafuta kusaidia kudhibiti bei kwa mda wa miezi 3 ijayo.

Kwa sasa serikali inasema kuna akiba ya kutosha ya mafuta na shehena zaidi zinatarajiwa nchini hivi karibuni.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading

Business

KPA yaimarisha usafirishaji wa makasha na kampeni za kimataifa

Published

on

By

Halmashauri ya bandari nchini (KPA), imeimarisha ushirikiano wake na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya bahari, Maersk, katika juhudi za kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika Mashariki.

Makubaliano hayo yameafikiwa katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya KPA jijini Mombasa ambapo Mkurugenzi wa Maersk Kanda ya Afrika Mashariki, Tito Okuku, alieleza kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua shughuli zake zaidi nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Moja ya maeneo yatakayopata kipaumbele ni kuimarisha matumizi ya Kituo cha Makontena cha ndani cha Naivasha kinachotazamwa kama kitovu muhimu katika kushughulikia usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka Kenya kwenda masoko ya kimataifa, huku kikitoa njia ya haraka na ya kuaminika kwa wauzaji kufikia masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kukubaliana na hatua hiyo akisema ni wakati mwafaka kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano huo.

Aidha alibainisha kuwa Bandari ya Mombasa pamoja na vituo vyake vya ndani vinaendelea kushuhudia ongezeko la shehena, na akahakikishia kuwa KPA iko tayari kushughulikia mahitaji yanayoongezeka kupitia maboresho ya miundombinu na huduma.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Trending