Sports
Mwanariadha Kipyegon Kutimka Chini Ya Dakika 4,Paris
Bingwa wa Olimpiki wa dunia mbio za mitaa 1500 Mkenya Faith Kipyegon atakua anaingia kwenye daftari za kumbukumbu kwa kuwa mwanamke wa kwanza kukimbia mile moja chini ya dakika nne mjini Paris Ufaransa.
Mkimbiaji huyo nguli na bingwa mara tatu wa Olimpiki ndiye mshilikizi wa rekodi bora zaidi ya mbio za mitaa 1500 na anatarajiwa kurejea katika mji wa Stade Charlety leo usiku kufanya vile.
Zaidi ya wanaume 200 wamekimbia mile moja kwa dakika nne mwanamke pekee ambaye amekaribia hapo ni Kipyegon ambaye alivunja rekodi yake mwenyewe wa mita 1500 mjini Monaco kwa muda bora wa dakika 4:07.64 mwaka 2023.
Mtimkaji huyo hata hivyo atakua anasaidiwa na vifaa maalum kwenye viatu katika shindano hilo la Break4 kama ilivyokua kwa nguli wa mbio za masafa marefu Eliud Kipchoge alipokimbia chini ya 2 mjini Vienna.
Iwapo atavunja rekodi hiyo atapokea shilingi milioni 13 pesa za kenya.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

