Sports
Simba SC yaikwatua Gor Mahia mechi ya kirafiki Uwanjani Benjamin Mkapa
Miamba wa soka nchini Tanzania klabu ya Simba waliwashinda mabingwa wa zamani wa ligi kuu nchini Kenya, Gor Mahia, mabao 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Jumatano jioni katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa.
Mchuano huo ulikuwa wa maadhimisho ya siku ya Simba Dei ambapo ni siku ya utambulisho wa wachezaji wapya kilabuni humo.
Wekundu wa Msimbazi Simba walijipatia magoli yao kupitia kwa beki Abdulrazak Hamza na mshambulizi wa raia wa Uganda Steven Dese Mukwala katika kila kipindi.
Timu zote zilitumia mechi hiyo kama maandalizi ya mwisho kabla ya kungoa nanga kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Kenya na ile ya Tanzania Bara.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

