Sports
Starlets Watambaa Dhidi Ya Crested Cranes Ya Uganda
Timu ya Taifa ya soka akina dada Harambee Starlets imeendeleza ilipoachia mechi ya pili taji la CECAFA ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kunyuka Crested Cranes ya Uganda kipigo cha magoli 4-0 mechi ya pili Ugani Azam Sports Complex mjini Dar es salaam Tanzania.
Kiungo wa kilabu ya Kenya Police Bullets Diana Wacera aliwaweka uongozini vipusa wa nyumbani kunako dakika ya 19,Huku nyae beki wa kimataifa Dorcas Shikhobe akiweka kambani goli la pili kunako dakika ya 27,mshambulizi wa kimataifa Violet Wanyonyi Nanjala akifunga goli la tatu dakika ya 29 naye kiungo wa kilabu ya Vihiga Queens Martha Amunyolet akifunga goli la nne na la mwisho dakika ya 81 kipindi cha pili.
Huu ukiwa ni ushindi wa pili kwa timu hiyo chini ya kocha Beldine Odemba katika mechi ya kwanza walishinda Burundi magoli 3-0 siku ya Jumapili.
Katika mechi nyingine Twiga Stars ya tanzania walirindima Burundi magoli 6-0 katika uga uo huo.Kituo kinachofuata kwa Starlets ni dhidi ya Sudan Kusini Alhamisi.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

