Sports
Timu Ya Harambee Stars imefuzu Robo Fainali Kipute Cha CHAN
Timu ya taifa soka Harambee stars wametinga kwenye hatua ya robo fainali taji la CHAN baada ya matokeo ya jana.
Timu ya Taifa ya Angola Palancas Negras imeungana na Zambia Chipolopolo kuaga michuano ya kombe la Mataifa Afrika kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wa Kundi A huku vinara Kenya (alama 7) wakitinga robo fainali kabila yamechi ya mwisho.
Morocco (alama 6) waliopo nafasi ya pili na DR Congo (alama 6) nafasi ya tatu watachuana kuwania nafasi moja ya kufuzu robo fainali kwenye michezo ya mwisho huku Kenya ikikamilisha ratiba kwa mchezo dhidi ya Washika Mkia, Zambia.