Business
Wakulima wa Mananasi Magarini walilia soko
Wakulima wa matunda aina ya nanasi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kuwatafutia soko ili kuuza bidhaa zao ambazo zinaendelea kuharibika msimu huu.
Kulingana na wakulima hao hakuna soko ambapo wanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nzuri hali inayofanya wakulima wengi kuuza kwa bei ya chini ili kuepuka kuharibika kwa katunda hayo.
Wakizunumza na cocofm wakulima hao walisema kuwa kwa sasa wanakadiria hasara kwani matunda ni mengi.
Wakati huo huo wakulima hao wameitaka serikali ya kaunti kujenga viwanda.
Ni kauli ambayo imeongwa mkono na wafanyibiashara wa matunda mjini Kilifi kaunti ya Kilifi ambao walisema kuwa matunda mengi msimu huu huharibika kutokana na idadi ndogo ya wateja.
“Serikali itutafutie soko pamoja na kujenga viwanda ili kusaidia wakulima na wafanyibiashara wa matunda aina ya mamanasi, kuuza matunda yao ili kuawaepushia hasara hasa wakati huu ambapo matunda ni mengi.”
Taarifa ya Pauline Mwango
Business
KPA yaimarisha usafirishaji wa makasha na kampeni za kimataifa
Halmashauri ya bandari nchini (KPA), imeimarisha ushirikiano wake na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya bahari, Maersk, katika juhudi za kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika Mashariki.
Makubaliano hayo yameafikiwa katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya KPA jijini Mombasa ambapo Mkurugenzi wa Maersk Kanda ya Afrika Mashariki, Tito Okuku, alieleza kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua shughuli zake zaidi nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.
Moja ya maeneo yatakayopata kipaumbele ni kuimarisha matumizi ya Kituo cha Makontena cha ndani cha Naivasha kinachotazamwa kama kitovu muhimu katika kushughulikia usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka Kenya kwenda masoko ya kimataifa, huku kikitoa njia ya haraka na ya kuaminika kwa wauzaji kufikia masoko ya kimataifa.
Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kukubaliana na hatua hiyo akisema ni wakati mwafaka kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano huo.
Aidha alibainisha kuwa Bandari ya Mombasa pamoja na vituo vyake vya ndani vinaendelea kushuhudia ongezeko la shehena, na akahakikishia kuwa KPA iko tayari kushughulikia mahitaji yanayoongezeka kupitia maboresho ya miundombinu na huduma.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
Business
Serikali yatenga milioni 838 kufidia waathiriwa wa soko la Mtwapa
Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni mbili kwa ajili ya fidia ya ardhi na shilingi milioni 838 kwa kuhamisha wafanyabiashara katika eneo la Mtwapa ili kufanikisha ujenzi wa barabara ya Mombasa–Kilifi.
Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa Daraja la Mtwapa, Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir alisema wafanyibiashara ambao wanaendeleza biashara zao katika soko la Mtwapa watahamishwa katika maeneo mengine ambapo wataweza kuendeleza biashara zao ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, wafanyabiashara walioko katika mji wa Mtwapa ambao wameathiriwa na upanuzi wa barabara wamepewa notisi ya siku 30 kuondoka ili kupisha kuanza kwa awamu inayofuata ya ujenzi, akieleza kuwa fedha zilizotengwa zinalenga kuhakikisha uhamishaji huo unafanyika kwa utaratibu unaozingatia sheria.
Aidha Chirchir aliongeza kuwa mradi unaendelea vyema, akisema kuwa ukikamilika utainua uchumi wa wafanyibiashara na eneo la Pwani kwa ujmla.
“Serikali imetenga shilingi milioni 838 zitakazohakikisha kuwa wafanyibiashara wanahamishwa katika njia nzuri na mazingira mazuri ili kupisha ujenzi wa barabara hivyo wafanyibiashara wote msiwe na wasiwasi wowote maana mikakati imewekwa.” alisema Chirchir.
Taarifa ya Pauline Mwango

