Connect with us

Business

Wavuvi Kwale wadai kuhangaishwa na wavuvi wa Tanzania

Published

on

Wavuvi kaunti ya Kwale walalamikia kukandamizwa na wavuvi kutoka taifa jirani la Tanzania kufuatia  mizozo ya mipaka.

Kulingana nao wavuvi hao, wamekua wakinyanyaswa  na hata kutozwa  faini ya hadi shilingi milioni 4 wanapopatikana wakivua katika sehemu zinazodaiwa kuwa katika nchi ya Tanzania  na maafisa hao.

Juma Rama Yusuf mwenyekiti wa wavuvi eneo la Jimbo na mwenzake wa Vanga Ngoto Mohamed walisema kuwa wavuvi wa Tanzania wamepewa  uhuru wa kutekeleza shughuli za uvuvi humu nchini ili hali wenyeji wanahangaika.

Aidha waliitaka  serikali ya  Kenya  na ile ya Tanzania  kuja pamoja na kutatua swala la  mipaka katika bahari hindi ili kukomesha mizozo ya mara kwa mara inaoshuhudiwa kati ya wavuvi wa Kenya na maafisa walinda bahari kutoka Tanzania.

 Taarifa ya Pauline Mwango

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

KPA yaimarisha usafirishaji wa makasha na kampeni za kimataifa

Published

on

By

Halmashauri ya bandari nchini (KPA), imeimarisha ushirikiano wake na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya bahari, Maersk, katika juhudi za kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika Mashariki.

Makubaliano hayo yameafikiwa katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya KPA jijini Mombasa ambapo Mkurugenzi wa Maersk Kanda ya Afrika Mashariki, Tito Okuku, alieleza kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua shughuli zake zaidi nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Moja ya maeneo yatakayopata kipaumbele ni kuimarisha matumizi ya Kituo cha Makontena cha ndani cha Naivasha kinachotazamwa kama kitovu muhimu katika kushughulikia usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka Kenya kwenda masoko ya kimataifa, huku kikitoa njia ya haraka na ya kuaminika kwa wauzaji kufikia masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kukubaliana na hatua hiyo akisema ni wakati mwafaka kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano huo.

Aidha alibainisha kuwa Bandari ya Mombasa pamoja na vituo vyake vya ndani vinaendelea kushuhudia ongezeko la shehena, na akahakikishia kuwa KPA iko tayari kushughulikia mahitaji yanayoongezeka kupitia maboresho ya miundombinu na huduma.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Business

Wakulima wa Mananasi Magarini walilia soko

Published

on

By

Wakulima wa matunda aina ya nanasi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kuwatafutia soko ili kuuza bidhaa zao ambazo zinaendelea kuharibika msimu huu.

Kulingana na wakulima hao hakuna soko ambapo wanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nzuri hali inayofanya wakulima wengi kuuza kwa bei ya chini ili kuepuka kuharibika kwa katunda hayo.

Wakizunumza na cocofm wakulima hao walisema kuwa kwa sasa wanakadiria hasara kwani matunda ni mengi.

Wakati huo huo wakulima hao wameitaka serikali ya kaunti kujenga viwanda.

Ni kauli ambayo imeongwa mkono na wafanyibiashara wa matunda mjini Kilifi kaunti ya Kilifi ambao walisema kuwa matunda mengi msimu huu huharibika kutokana na idadi ndogo ya wateja.

“Serikali itutafutie soko pamoja na kujenga viwanda ili kusaidia wakulima na wafanyibiashara wa matunda aina ya mamanasi, kuuza matunda yao ili kuawaepushia hasara hasa wakati huu ambapo matunda ni mengi.”

Taarifa ya Pauline Mwango

Continue Reading

Trending