Sports
William Saliba asaini mkataba mpya na Arsenal kwa miaka mitano ijayo
Beki wa taifa la Ufaransa William Saliba amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na kilabu yake ya Arsenal na kusitisha uvumi wa kuondoka Emirate hivi karibuni.
Haya yanajiri Baada ya makubaliano ya maneno wiki iliyopita, beki huyo wa Kifaransa sasa ameweka kalamu karatasi na kujifunga kwa mradi wa muda mrefu wa Arsenal.
Saliba, ambaye alikuwa akivutiwa na vilabu vikubwa ikiwemo Real Madrid kwa mwaka 2026, ameamua kujitolea mustakabali wake Emirates.
Ni taarifa nzuri kwa Arsenal wanaona hii kama hatua muhimu ya kuimarisha safu ya ulinzi kwa muda mrefu kwani beki huyo amekua nguzo muhimu katika kikosi hicho chini ya kocha Mikel Arteta ambao pia wamesajili mabeki wawili Christian Mosquera na Piero Hincapie,
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

