Sports

Malkia Strikers Watangaza Kikosi cha Mwisho cha Wachezaji 14 kwa Kombe la Dunia la Voliboli FIVB 2025 Nchini Thailand

Published

on

Shirikisho la Voliboli nchini Kenya (KVF) mapema leo limetangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 14 wa Malkia Strikers kitakachoshiriki mashindano ya Dunia ya FIVB 2025 yatakayofanyika kuanzia Agosti 22 hadi Septemba 7 nchini Thailand.

Jumla ya wachezaji 17 walikuwa kwenye kambi ya mazoezi ya ndani katika ukumbi wa mazoezi wa Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Wakati huo huo, wachezaji wawili wamejumuishwa kama washirika wa mazoezi, nao ni mshambuliaji wa upande wa nje wa DCI Sarah Namisi na mzuiaji wa kati wa Kenya Pipeline, Marriane Sokoiyo.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Vietnam kwa mechi za kirafiki dhidi ya Vietnam na Uhispania kabla ya kuelekea Thailand tarehe 20 Agosti kwa ajili ya mashindano ya dunia. Timu hiyo itasafiri kwa awamu mbili; kundi la kwanza liliondoka Alhamisi usiku huku kundi la pili likitarajiwa kuondoka Ijumaa.

Kenya imepangwa Kundi “G” pamoja na Poland, Ujerumani na Vietnam.

Wakati wa kutangazwa kwa kikosi hicho, alikuwapo pia Frank Ochieng, Meneja Masoko wa Mozart Bet ambaye ni mdhamini mkuu wa Malkia Strikers.


Kikosi cha Malkia Strikers:

  • Wapigaji mipira (Setters): Emmaculate Nekesa, Fridah Boke

  • Wakombozi (Liberos): Cellestine Nyongesa, Sharleen Maywa

  • Washambuliaji wa kushoto: Juliana Namutira, Meldine Sande (nahodha), Veronica Adhiambo, Daisy Leting

  • Washambuliaji wa kulia: Pamela Adhiambo, Mercy Iminza, Marlyne Tata

  • Wazuiaji wa kati (Middle blockers): Gladys Ekaru (naibu nahodha), Belinda Barasa, Lorraine Chebet

  • Washirika wa mazoezi: Sarah Namisi na Marriane Sokoiyo

Maafisa wa Timu:

  • Kocha Mkuu – Geoffrey Omondi

  • Makocha Wasaidizi – David Muthui, Esther Jepkosgei

  • Mkufunzi wa viungo – Mavisi Azenga

  • Mkuu wa msafara – Paul Bitok

  • Mlezi wa Timu – Neddy Nelimo

  • Mtaalamu wa tiba ya viungo – Sarah Karongo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version