Sports
Mchezaji Tenesi Alcaraz Bingwa Tena
Mchezaji Tenesi anayeorodheshwa wa Pili duniani kwa sasa Carlos Alcaraz raia wa Uhispania ameweza kuandikisha rekodi mpya baada ya kushinda taji la pili kombe la Queens Cup Title baada ya kumlaza Jiri Licheka raia wa Czech kwa seti za 7-5, 6-7 (5/7), 6-2 kabila ya finali ya Wimblendon.
Nyota huyo raia wa Uhispania alimzidi mwenzake kwenye fainali baada ya kuonyesha makali tokea mwanzo huku mchezaji huyo anayeorodheshwa wa 30 akikubali kichapo hicho kwa muda lisali 2 na dakika 10.
Mwanatenesi huyo tayari ana mataji matano baada ya kuzishinda fainali za French Open,Rome Open,Monte Carlo na Rotherdam mwaka huu wa 2025.
Mwamba huyo hajapoteza katika mashindano fainali 18 mpaka sasa tangu fainali za Barcelona Open April 20.
Entertainment
Arsenal Ikishinda Kombe Nitampa Main Man Rio Gari na Dadangu – Shuga Boy
Mjadala mkali umeibuka katika kipindi cha COCO Asubuhi baada ya Shuga Boy, shabiki wa Manchester United, kuweka dau zito na la kushangaza dhidi ya Main Man Rio ambaye ni shabiki wa Arsenal.
Akizungumza kwenye kipindi cha COCO Asubuhi, kinachoendeshwa na Tatu Sure—inayojumuisha Shuga Boy mwenyewe, Main Man Rio na Solomon Zully—Shuga Boy alifunguka, akidai kuwa Arsenal hawana uwezo wa kubeba hata kombe moja msimu huu licha ya matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki wao.
Kwa mujibu wa Shuga Boy, mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakijipa matumaini makubwa ya kutwaa hadi vikombe vinne, lakini hali halisi uwanjani haioneshi dalili hizo. Alienda mbali zaidi na kuweka dau la kipekee kwa Main Man Rio, ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal.
“Nilimwambia Main Man Rio, wakibeba kombe nitampa gari yangu. Sasa naongeza dau—wakishinda kikombe msimu huu, nitampa gari yangu pamoja na dadangu,” alisema Shuga Boy kwa msisitizo, kauli iliyozua kicheko na mjadala mkali studio.
Kauli hiyo imekuja katika kipindi ambacho Arsenal wamekuwa wakionyesha ushindani mkubwa chini ya kocha Mikel Arteta, wakijijenga kama moja ya timu zinazowania ubingwa wa Premier League. Licha ya maendeleo hayo, ukosefu wa vikombe katika misimu mingi bado unawapa wapinzani wao nafasi ya kuwabeza.
Kwa upande mwingine, Manchester United nao wanapitia kipindi cha mabadiliko, wakijaribu kurejea kwenye ubora wao wa zamani waliouonyesha enzi za Sir Alex Ferguson. Licha ya changamoto, bado wana historia nzito ya mafanikio, jambo linalowapa mashabiki wao kujiamini wanapojadili soka la Uingereza.
Usiku wa leo, macho ya mashabiki yataelekezwa kwenye mchezo wa ligi kati ya Manchester United dhidi ya Leeds United—mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku Shuga Boy akitumaini timu yake itapata ushindi na kuendeleza presha kwa wapinzani wao.
Wakati mabishano yakiendelea mitandaoni na kwenye studio za redio, swali kubwa linabaki: Je, Arsenal wataweza kuwanyamazisha wakosoaji wao kwa kubeba angalau kombe moja msimu huu, au kauli ya Shuga Boy itageuka kuwa unabii?

