Connect with us

News

Mwadime, Amewataka Vijana Kujisajili na Vyuo vya Kiufundi

Published

on

Katibu katika Wizara ya Leba nchini Shadrack Mwadime amewataka vijana ambao wana ujuzi mbalimbali lakini hawana stakabadhi kujisajili na Mamlaka ya kitaifa ya mafunzo ya viwanda NITA ili waweze kupata vyeti na ajira. 

Kulingana na Mwadime, Mamlaka ya NITA imekuwa mstari wa mbele katika kutoa vyeti ambavyo wakenya wanaweza kupata ajira katika mataifa ya ughaibuni na zenye malipo bora.

Akizungumza wakati wa kutoa vyeti hivyo kwa wanafunzi wa chuo cha kiufundi cha Dzitsoni katika kaunti ya Kilifi, Mwadime amesema tayari kuna wanafunzi zaidi ya elfu 20 ambao wamesajiliwa kufanya mitihani katika Mamlaka hiyo ili waweze kupata vyeti hivyo. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa kamati ya Leba katika bunge la kitaifa ambaye pia ni mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga, amewahimiza vijana kujiunga na vyuo vya kiufundi huku Mwenyekiti wa bodi ya Mamlaka ya NITA Aden Noor Ali akisema kila mwaka wanahamasisha wanafunzi zaidi ya laki moja kujisajili na NITA.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

ODM yatishia kujiondoa katika serikali jumuishi

Published

on

By

Huenda mpango wa serikali jumuishi uliobuniwa na rais William Ruto na aliyekuwa Kinara wa chama cha ODM hayati Raila Odinga ukavunjika iwapo masuala ibuka yaliyowasilishwa na Chama cha ODM yatakosa kutimizwa.

Chama hicho kimekosoa jinsi baadhi ya wafuasi wa chama cha UDA kujitenga na mwenzao wa ODM licha ya kuwepo na mpango wa serikali jumuishi pamoja na kukosoa kutishiwa kwa baadhi ya viongozi wa ODM kujiondoa na chama hicho ili wajiunge na UDA.

Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa Junet Mohammed alisema kuna njama ya kusambaratishwa kwa ushawishi wa chama cha ODM katika maeneo ya Nyanza na Pwani kwani kuna taarifa kwamba baadhi vya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakishurutishwa na maafisa wa Ikulu ya rais.

Junet ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki, alisisitiza kwamba ODM kujiunga na UDA haikuwa na makusudi bali serikali ilihitaji msaada wa viongozi wa chama hicho ili kulinusuru taifa kwani lilikuwa linaelekea mahali pabaya.

“Hatuko kwa serikali jumuishi kimakosa ama kimakusudi wala kwa mualiko bali tuliingia katika serikali jumuishi kutokana na serikali ya rais Ruto kutaka msaada watu ili kulinusuru taifa lakini kama uongozi wa UDA unaona kumetengeza misingi na umaarufu mashinani tunaweza kuwaacha watengeze serikali yao mwaka 2027”, alisema Junet.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Mwanachama wa Kamati kuu ya chama hicho alisema wataisha mkutano wa dharura wa Kamati kuu ili kuangazia suala hilo kwani mvutano huo huenda ukazidi kushamiri iwapo hakutakuwa na mikakati mwafaka.

Katika siku za hivi majuzi katika siasa za mashinani, chama cha UDA kimeonekana kikiendeleza siasa za kuimarisha chama hicho pamoja na kusajili wanachama wapya ili kujienga umaarufu zaidi kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Viongozi wa UDA walionekana kutangaza hadharani kwamba hakutakuwa na mpango wa kusimamisha mgombea mmoja katika eneo kwenye serikali jumuishi yaani Zoning bali kila kiongozi akijipange kisiasa na kupambana katika nyadhfa anayoelenga kushikilia wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Polisi wanachunguza tukio la wizi dhidi ya raia wa kigeni

Published

on

By

Maafisa wa Polisi kaunti ya Mombasa wanachunguza tukio la wizi dhidi ya mtalii wa kigeni lililotokea katika eneo la Nyali

Kulingana na ripoti ya maafisa wa polisi, mtalii huyo mwenye umri wa miaka 51 ambaye ni raia wa Marekani, anadai kulaghaiwa na kisha kushambuliwa na kundi la wanaume aliyokutana nao muda mfupi kabla ya tukio.

Ripoti hiyo imeeleza kwamba mnamo mwezi Aprili 9 mwaka huu, raia huyo wa kigeni akiwa katika mkahawa mmoja eneo la Nyali jijini Mombasa, alikutana na mwanaume aliyejitambulisha kama Alex, ambaye alimshawishi kuelekea katika nyumba ya Airbnb iliyoko karibu na mkahawa huo.

Taarifa hiyo ilifafanua zaidi kwamba alipofika katika chumba hicho, alikumbana na wanaume wengine watano waliokuwa wakimsubiri ambapo mlango ulifungwa na kisha akashambuliwa na kulazimishwa kutoa pesa na vitu vya thamani.

Wahalifu hao walitoroka na mali mbalimbali ikiwemo simu ya rununu, kompyuta mpakato (laptop), fedha taslimu pamoja na fedha za kigeni na pia walifanikiwa kutoa pesa kutoka kwenye kadi zake za benki kwa njia ya udanganyifu.

Maafisa wa polisi kutoka Bamburi kwa kushirikiana na maafisa wa upelelezi wa DCI Nyali walifika eneo la tukio na kuanza uchunguzi, ingawa hadi sasa hakuna mtu aliyekamatwa wala mali iliyopatikana.

Kesi hiyo imewekwa chini ya uchunguzi zaidi huku juhudi zikiendelea kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Trending