Connect with us

Business

Wadau wa utalii Watamu waunga mkono ada za maegesho mbugani

Published

on

Wadau wa sekta ya Utalii eneo la Watamu kaunti ya Kilifi wameunga mkono pendekezo la shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS la kutathmini upya ada za kuegesha magari mbugani.

Wadau hao walitoa shinikizo kuwa mabadiliko hayo yaainishwe na huduma zilizoboreshwa vile vile matokeo ya uhifadhi mbugani.

Wakizungumza wakati wa kikao cha kubadilishama maoni kuhusu suala hilo mjini Watamu, Patrick Changawa, mmoja wa wahudumu wa safari za kitalii, alisistiza kuhusu mchango muhimu unaotolewa na sekta ya utalii katika uchumi wa taifa.

Alipongeza KWS kwa kushirikisha wahusika wamaeneo hayo katika mchakato wa mashauriano.

“KWS imetuhamasisha kuhusu namna ada za uhifadhi zilizofanyiwa ukarabati zitakavyoanza kutekelezwa, mgao mkubwa wa fedha utatumika katika kuimarisha mbuga za baharini kupitia urejeshaji wa miamba ya matumbawe, udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, na programu za kufikia jamii,” alisema Changawa.

Mkurugenzi msaidizi wa eneo la hifadhi ya pwani katika KWS Elema Hapicha alibainisha kuwa vikao sawa vya ushirikishwaji wa umma vinafanyika nchini kote ili kukusanya maoni kutoka kwa wadau.

“Wadau wa Watamu wametoa maoni muhimu kuhusu rasimu ya muundo wa ada ya uhifadhi,” Hapicha alisema.

Mapendekezo hayo yamejikita katika rasimu ya kanuni za uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori (Ada ya Ufikiaji na Uhifadhi) za 2025.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

KPA yaimarisha usafirishaji wa makasha na kampeni za kimataifa

Published

on

By

Halmashauri ya bandari nchini (KPA), imeimarisha ushirikiano wake na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya bahari, Maersk, katika juhudi za kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika Mashariki.

Makubaliano hayo yameafikiwa katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya KPA jijini Mombasa ambapo Mkurugenzi wa Maersk Kanda ya Afrika Mashariki, Tito Okuku, alieleza kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua shughuli zake zaidi nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Moja ya maeneo yatakayopata kipaumbele ni kuimarisha matumizi ya Kituo cha Makontena cha ndani cha Naivasha kinachotazamwa kama kitovu muhimu katika kushughulikia usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka Kenya kwenda masoko ya kimataifa, huku kikitoa njia ya haraka na ya kuaminika kwa wauzaji kufikia masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kukubaliana na hatua hiyo akisema ni wakati mwafaka kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano huo.

Aidha alibainisha kuwa Bandari ya Mombasa pamoja na vituo vyake vya ndani vinaendelea kushuhudia ongezeko la shehena, na akahakikishia kuwa KPA iko tayari kushughulikia mahitaji yanayoongezeka kupitia maboresho ya miundombinu na huduma.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Business

Wakulima wa Mananasi Magarini walilia soko

Published

on

By

Wakulima wa matunda aina ya nanasi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kuwatafutia soko ili kuuza bidhaa zao ambazo zinaendelea kuharibika msimu huu.

Kulingana na wakulima hao hakuna soko ambapo wanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nzuri hali inayofanya wakulima wengi kuuza kwa bei ya chini ili kuepuka kuharibika kwa katunda hayo.

Wakizunumza na cocofm wakulima hao walisema kuwa kwa sasa wanakadiria hasara kwani matunda ni mengi.

Wakati huo huo wakulima hao wameitaka serikali ya kaunti kujenga viwanda.

Ni kauli ambayo imeongwa mkono na wafanyibiashara wa matunda mjini Kilifi kaunti ya Kilifi ambao walisema kuwa matunda mengi msimu huu huharibika kutokana na idadi ndogo ya wateja.

“Serikali itutafutie soko pamoja na kujenga viwanda ili kusaidia wakulima na wafanyibiashara wa matunda aina ya mamanasi, kuuza matunda yao ili kuawaepushia hasara hasa wakati huu ambapo matunda ni mengi.”

Taarifa ya Pauline Mwango

Continue Reading

Trending