Connect with us

Business

Walimiki wa hoteli za kitalii Kilifi wapewa changamoto

Published

on

Wamiliki hoteli zilizofungwa kaunti ya Kilifi wameshinikizwa kuhakikisha wanaziuza kwa wawekezaji wengine iwapo wameshindwa kurejesha huduma katika hoteli hizo.

Akizungumza na vyombo vya habari gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuhakikisha sekta ya utalii inaimarika ikizingatiwa kwamba ni mojawapo ya kitega uchumi cha kaunti hii ya Kilifi.

Aidha gavana Mung’aro ameeleza matumaini ya kuimarika kwa sekta hiyo baada ya kupatikana kwa masoko kwenye mataifa mbalimbali ya ulaya.

Kwa upande wake waziri wa utalii na biashara kaunti ya Kilifi Raymond Ngala amehoji kuwa serikali ya kaunti itajizatiti kuboresha sekta hiyo hasa kupitia wa michezo.

Ngala amesema kuwa sekta ya utalii iko na uwezo wa kubuni nafasi nyingi za ajira kwa vijana na kupunguza changamoto ya ukosefu ajira, hivyo serikali itahakikisha kuwa sekta hiyo inaboreshwa.

“Wale wenye hoteli ambao wanashindwa kuendeleza biashara hiyo wapeane hoteli hizo kwa wawekezaji wengine ili kuendeleza shughuli badala ya kuziacha bila kuendelea ikizingatiwa kuwa uchumi wa kaunti hii unategemea hoteli hizo kupokea wageni.” alisema Ngala.

Taarifa ya Pauline Mwango.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Business

KPA yaimarisha usafirishaji wa makasha na kampeni za kimataifa

Published

on

By

Halmashauri ya bandari nchini (KPA), imeimarisha ushirikiano wake na kampuni ya kimataifa ya usafirishaji kwa njia ya bahari, Maersk, katika juhudi za kuboresha huduma na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo katika eneo la Afrika Mashariki.

Makubaliano hayo yameafikiwa katika mkutano uliofanyika katika makao makuu ya KPA jijini Mombasa ambapo Mkurugenzi wa Maersk Kanda ya Afrika Mashariki, Tito Okuku, alieleza kuwa kampuni hiyo ina nia ya kupanua shughuli zake zaidi nchini na katika eneo la Afrika Mashariki kwa ujumla.

Moja ya maeneo yatakayopata kipaumbele ni kuimarisha matumizi ya Kituo cha Makontena cha ndani cha Naivasha kinachotazamwa kama kitovu muhimu katika kushughulikia usafirishaji wa mazao ya kilimo kutoka Kenya kwenda masoko ya kimataifa, huku kikitoa njia ya haraka na ya kuaminika kwa wauzaji kufikia masoko ya kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa KPA, Nahodha William Ruto, alieleza kukubaliana na hatua hiyo akisema ni wakati mwafaka kwa pande zote mbili kuimarisha ushirikiano huo.

Aidha alibainisha kuwa Bandari ya Mombasa pamoja na vituo vyake vya ndani vinaendelea kushuhudia ongezeko la shehena, na akahakikishia kuwa KPA iko tayari kushughulikia mahitaji yanayoongezeka kupitia maboresho ya miundombinu na huduma.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Business

Wakulima wa Mananasi Magarini walilia soko

Published

on

By

Wakulima wa matunda aina ya nanasi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wanaitaka serikali kuwatafutia soko ili kuuza bidhaa zao ambazo zinaendelea kuharibika msimu huu.

Kulingana na wakulima hao hakuna soko ambapo wanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nzuri hali inayofanya wakulima wengi kuuza kwa bei ya chini ili kuepuka kuharibika kwa katunda hayo.

Wakizunumza na cocofm wakulima hao walisema kuwa kwa sasa wanakadiria hasara kwani matunda ni mengi.

Wakati huo huo wakulima hao wameitaka serikali ya kaunti kujenga viwanda.

Ni kauli ambayo imeongwa mkono na wafanyibiashara wa matunda mjini Kilifi kaunti ya Kilifi ambao walisema kuwa matunda mengi msimu huu huharibika kutokana na idadi ndogo ya wateja.

“Serikali itutafutie soko pamoja na kujenga viwanda ili kusaidia wakulima na wafanyibiashara wa matunda aina ya mamanasi, kuuza matunda yao ili kuawaepushia hasara hasa wakati huu ambapo matunda ni mengi.”

Taarifa ya Pauline Mwango

Continue Reading

Trending