Connect with us

News

Bunduki 90 zasalimishwa kwa Polisi kaunti ya Tana River

Published

on

Takribani bunduki 90 ambazo zilikuwa zikimiliwa na watu kinyume cha sheria zimesalimishwa kwa maafisa wa polisi katika kaunti ya Tana River.

hatua hiyo imetokana na oparesheni ya kiusalama iliyofanywa na maafisa wa polisi ambayo inaendelezwa hadi sasa katika maeneo ya Tana Kaskazini na Bangale kutokana na vita vya kikabila ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa katika maeneo hayo.

Vita vya kikabila katika eneo la Bangale kaunti ya Tana River, mara nyingi hutokea kati ya jamii za wafugaji kama vile jamii za Wardey, Degodia na Orma huku serikali kupitia idara ya usalama ikiingilia kati ili kuhakikisha jamii hizo zinaishi kwa amani.

Mizozo hii huibuka hasa kutokana na ushindani wa kupata malisho na maji kwa ajili ya mifugo wao, mizozo ya ardhi, na uchochezi wa kisiasa kuelekea chaguzi.

Serikali imezitaka jamii hizo kuzidi kuwasilisha silaha zote kwa maafisa wa polisi, ili kuzuia vita vya kila mara sawa na kuchangia amani na umoja katika jamii hizo.

Kwa muda mrefu kaunti ya Tana River imekuwa ikishuhudia vita vya kikabila kila mara kwa mara kutokana na umiliki haramu wa silaha hali ambayo imechangia usalama wa kaunti hiyo kuwa duni.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

NCTC yaanzisha hamasa mashinani kudhibiti ugaidi

Published

on

By

Kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugaidi yaani National Counter Terrorism Centre (NCTC) kimeanzisha mpango wa kutoa hamasa za kuwaepusha wananchi na masuala ya ugaidi hasa maeneo ya Shakahola katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.

Akizungumza katika eneo hilo, Afisa mkuu wa kituo hicho Grace Kaparo aliwataka wazazi kufuatilia kwa ukaribu mienendo ya watoto wao kama njia mojawapo ya kuzuia michipuko ya makundi ya ugaidi.

Kaparo alidokeza kwamba mpango huo unalenga kupunguza visa vya uhalifu miongoni mwa vijana sambamba na kuwajengea mustakabali bora wa maisha yao.

Hamasa hiyo inajiri baada ya kushughudiwa maafa ya watu zaidi ya 400 katika msitu wa Shakahola kutokana na mafunzo ya itikadi kali huku mshukiwa mkuu wa mauaji hayo akiwa katika mikono ya maafisa wa polisi.

“Tumekuja Shakahola kuelimisha jamii kuepusha makundi ya kigaidi na jinsi ya kutambua watu walio na itikadi kali ili kuepusha watu kuangamia kama hapa Shakahola watu wangekuwa na ufahamu wangeepuka maafa”, alisema Grace.

Kwa upande wake Naibu Kamishna eneo Malindi kaunti ya Kilifi Harrison Matevwa aliwataka maafisa wa utawala eneo hilo kuendeleza hamasa za mara kwa mara kwa wakaazi wa maeneo yao ili kutathmini changamoto zinazowakumba na kuzitatua mara moja.

“Naiambia kamati ya usalama eneo hili kutembea na kufanya baraza za usalama kuweza kuskia ile wananchi wanapitia kwa sababu wengi wanakosa usaidizi ndio watu wahalifu wakija wanaweza kuwapotosha”alisema Harrison.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Wakurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Direct Line waagizwa kufika Mahakamani

Published

on

By

Mahakama ya Malindi imewaamuru wakurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Direct Line kufika Mahakamani binafsi kwa ajili ya kuhojiwa.

Hii ni baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama ya kulipa fidia ya shilingi milioni 2.26 kwa mwanamke aliyejeruhiwa vibaya katika ajali ya barabarani iliyokea Oktoba 6, mwaka 2016.

Kampuni hiyo, inayohusishwa na familia ya mfanyabiashara mashuhuri nchini ilishindwa kumlipa Hellen Waiyaki kiasi cha shilingi 2,259,825 kama ilivyoamriwa na Mahakama.

Waiyaki aliwasilisha kesi Mahakamani baada ya kampuni hiyo kukosa kutekeleza wajibu wake wa kulipa kiwango hicho cha pesa licha ya kuagizwa na Mahakama kufuatia ajali hiyo iliyohusisha basi la Tahir Sheikh Said Transporters Limited, maarufu kama TSS Bus Company, yenye nambari ya usajili KBZ 475S.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Malindi, Joy Wesonga, alisema ni lazima wakurugenzi hao wafike Mahakamani binafsi na kujieleza, akisema kampuni hiyo imekuwa ikiwazuia wananchi kufikia ofisi zao.

“Wakurugenzi hao watahitajika kufika mahakamani wakiwa na kuwasilisha vitabu vya hesabu vilivyokaguliwa vya kampuni, taarifa za benki pamoja na sajili ya mali za kampuni kwa kipindi cha miaka miwili ya mwisho ya kifedha ili Mahakama iweze kubaini uwezo wa kifedha wa kampuni hiyo na hali ya shughuli zake za kibiashara nchini Kenya.” alisema Hakimu Wesonga.

Katika hati kiapo kilichowasilishwa mahakamani kupitia wakili wake George Wakahiu, Hellen Waiyaki alisema alikuwa abiria ndani ya gari hilo ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa uzembe kabla ya kupinduka na kusababisha ajali iliyomwacha na majeraha mabaya mwilini.

Kesi hiyo itaendeleza mnamo Julia 31 mwaka huu

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Continue Reading

Trending