Sports
Liverpool Kuwasilisha Ofa Mpya Kusajili Wirtz
Mabingwa wapya wa ligi ya Epl liverpool inatarajiwa kuwasilisha ofa nyingine kusaka hudumza kiungo matata wa Ujerumani Florian Wirtz.
Hii ni Baada ya kilabu ya Bayer Leverkusen kukataa ofa ya pauni milioni 113 kutoka kwa usajli wa mchezaji huyo ambaye ameweka wazi yuko tayari kujiunga na The Reds msimu ujao.
Leverkusen imeshikilia kuwa inahitaji kitita cha pauni milioni 126 kumwachilia nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia anamezewa mate na Real Madrid ya Uhispania na Manchester City wa Uingereza.
Inaaminika mchezaji huyo ndiye atakua sajili wa kwanza kwa kocha mkuu Arne Slot msimu huu wakiwa tayari kuwachiliwa nyota wake akiwemo mshmabulizi Darwin Nunez,Federico Chiesa,Harvey Elliot na Kostas Tsimiskas ambao wote wataondoka ugani Anfield.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

