News
Kenya yaadhimisha sherehe za 63 za Madaraka
Rais William Samoei Ruto amewaongaza wakenya kuadhimisha sherehe za kitaifa za 63 za Madaraka katika kaunti ya Wajir.
Hatua hii ni ya kihistoria kuwa kufanyika katika kaunti ya Wajir tangu taifa lijipatie uhuru kinyume na maeneo mengine ya taifa hili la Kenya.
Kaunti ya Wajir ni kati ya kaunti zinazopatika katika maeneo ya Kaskazini mwa Kenya na maeneo ambayo mara nyingi yamekuwa yakishuhudia misururu ya mashambulizi ya kigaidi, lakini kutoka na serikali kuchukua hatua ya kuimarisha usalama katika maeneo hayo, sasa wakaazi wa kaunti hizo wamaanza kushuhudia matunda miradi ya maendeleo.
Wakati wa halfa hiyo iliyohudhuria na wakenya zaidi ya elfu 10 katika wanja wa Wajir Stadium, rais William Ruto ambaye ni amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi nchini, amesema atahakikisha sherehe za kitaifa zinafanyika katika kaunti mbalimbali nchini kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika hotuba yake kwenye sherehe hizo za Madaraka, Rais Ruto amesema tangu taifa la Kenya kupata uhuru eneo hilo lilitelekezwa katika masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Rais William Ruto awaongoza wakenya kuadhimisha sherehe za Madaraka kaunti ya Wajir
Rais Ruto pia alisema eneo hilo lilitengwa kwa miaka mingi kwa madai ni eneo kame na hakuna usalama wa kutosha.
“Katika uongozi wangu, nitahakikisha wananchi wa maeneo haya wanapata maendeleo sawa na wengine nchini, na niko na uchunguzi sana kuona watu wa Wajir wametengwa kwa miaka mingi na suala hili halitashuhudiwa tena na usalama utaimarishwa kwa wananchi wote”, alisema Rais
Wakati huo huo, Rais Ruto alisema kila jamii ina haki ya kunufaika na maendeleo nchini bila kubaguliwa na kuomba msamaha wenyeji wa kaunti ya Wajir kwa kutelekezwa kwa miaka mingi.
News
Mbunge wa Nyali amepuzilia mbali madai ya kuhusishwa na siasa za ukabila
Mbunge wa Nyali kaunti ya Mombasa Mohamed Ali amepuzilia mbali madai ya kuhusishwa na siasa za ukabila kwenye kaunti hiyo, akisema anafanya siasa zake bila kujali dini, kabila au hata eneo.
Akizungumza huko Nyali, Ali alisema kuna baadhi ya viongozi katika kaunti ya Mombasa, ambao wamekuwa wakiendekeza propaganda za kumhusisha na siasa za migawanyiko ili kumharibia jina taifa linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao wa 2027.
Ali ambaye alitangaza kuwania wadhifa wa ugavana kaunti ya Mombasa, aliwataka viongozi kufanya siasa zao kwa kunadi sera zao kwa wakaazi na maendeleo ambayo watatekeleza na sio kutumia suala la ukabila kuwachafulia wengine jina.
“2017 hakuna mtu aliniita mkabila, 2022 hakuna mtu aliniita mkabila, 2027 wanasema Mohamed Ali ni mkabila.Mimi Mohamed Ali, mimi nauliza nikisimama hapa juu ya gari, niseme kabila zote za Kenya wanaweza pewa nafasi ya ugavana ni kuna makosa?,basi sasa wanazunguka wakisema Mohamed ni mkabila kwasababu ameanza kufungua watu macho’’ alisema Ali.
Aidha, Ali alisema ataendelea kuzuru maeneo mbalimbali ya kauti ya Mombasa kunadi sera zake na kuwataka wakaazi wa kaunti hiyo kuwachagua viongozi wanaofaa ambao wataimarisha kaunti hiyo kimaendeleo.
‘’Mimi nimewaambia nitatembea hii Mombasa kwa uwezo wake mwenyezi mungu kutetea wananchi wa Mombasa’’ aliongeza Ali
Taarifa ya Janet Mumbi
News
Wakimbizi nusu milioni wakabiliwa na baa la njaa, Dadaab
Ripoti iliyotolewa hivi karibu na Shirika la Chakula duniani WFP ilionyesha kwamba zaidi ya wakimbizi nusu milioni wanaoishi katika kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab zilizoko nchini Kenya, wako katika hatari ya kuangamia kutokana na baa la njaa.
Kambi hizi ambazo zinahifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka nchini Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Somalia, ziko hatari iwapo zitakosa misaada ya chakula.
Kufuatia hali hiyo ambayo pia imechangiwa na mashirika ya kimataifa kusitisha ufadhili, sasa hali huenda ikawa tofauti baada ya taifa la Korea kwa ushirikiano na Kenya kutoa ufadhili wa shehena ya nafaka ya zaidi ya tani elfu 10 ambayo inakadiriwa kuwa kima cha shilingi milioni 1.2.
Katibu katika Idara ya uhamiaji nchini Belio Kipsang, aliyepokea msaada huo wa Chakula mjini Mombasa na kuhifadhiwa katika maghala ya Shirika la WFP, ameonya kwamba iwapo Kenya itakosa kupokea msaada kutoka kwa washirika na wafadhili wengine, basi italazimika kuchukua maamuzi magumu, ikiwemo kuwaondoa baadhi ya wakimbizi.
“Nyuma ya kila takwimu kuna familia ambazo ustahimilivu wao unaendelea kujaribiwa kila siku: akina mama wanaokosa kula ili watoto wao wapate chakula, watu walio katika mazingira hatarishi wakiruka milo, na vijana wanaokabiliwa na mustakabali usio na uhakika. Hizi si takwimu za kufikirika. Zinawakilisha watu halisi ambao heshima yao, afya yao na matarajio yao ya maisha yanategemea maamuzi tunayofanya kwa pamoja,” alisema.
Wakati wa hafla hiyo ya kupokea msaada huo wa chakula kwa wakimbizi wa Kakuma na Dadaab, Mkurugenzi wa Shirika la WFP nchini Kenya Betty Ka, alisema shehena ya nafaka itasaidia kuwahudumia takribani wakimbizi nusu milioni katika miezi ijayo.
“Usafirishaji huu unaonyesha umuhimu wa ushirikiano imara katika mnyororo wa ugavi wa misaada ya kibinadamu, ambapo ushirikiano huu kati ya Kenya, Mamlaka ya bandari Kenya (KPA), Shirika la viwango la Kenya(KEBS) na mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa kuhakikisha kwamba chakula cha msaada kinafanikishwa”,alisema Betty.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

