Sports
Msururu Wa Raga Driftwood 7s Umengoa Nanga Mombasa
Mashindano ya kitaifa ya misururu ya Raga nchini mwaka 2025 yameongoa nanga mjini Mombasa, Msururu huo wa kwanza wa Driftwood 7s inafanyika katika uwanja wa Mombasa Sports Club.
Jumla ya timu 26 zinashiriki katika makundi ya wavulana na wasichana wa chini ya umri wa miaka 18 na 15, na kundi la pamoja kwa walio chini ya miaka 13, yakionyesha kizazi kipya cha vipaji vya raga nchini Kenya.
Katika mashindano ya Divisheni ya Kwanza, mabingwa watetezi Kenya Harlequins wako Kundi A dhidi ya MMUST, KU Blak Blad, na Mwamba RFC,
Kundi B linajumuisha Kabras Sugar RFC,Catholic Monks, Nakuru RFC, na Impala RFC, kundi C linajumuisha KCB RFC, Nondescripts RFC, Daystar Falcons, na wenyeji MSC Rugby huku Kundi D litakuwa na ushindani mkali kati ya Menengai Oilers, Strathmore Leos, Stallions Rugby, na Kabarak University.
Kwa upande wa Division Two, timu 36 zinashiriki katika mashindano hayo, ambapo vigezo maalum vilitumika kugawa nafasi kwa vilabu wanachama wa KRU, timu kutoka ukanda wa pwani, zile zilizofanya vizuri awali, na zile zenye historia nzuri katika mashindano.
Makundi ya Division Two ni pamoja na AP Warriors, Kilifi Titans, Likoni, na Mean Machine ambao watacheza katika Kundi A; Embu RFC, Kaya Rugby, North Coast Stormers, na MKU Thika katika Kundi B; Homeboyz RFC, Jackals, NYS Eagles, na Makueni RFC katika Kundi C; Kisumu RFC, KCNP, NYS Spades, na Sigalagala NP katika Kundi D; huku South Coast Pirates, Vihiga Granites, Zetech Oaks, na Northern Suburbs wakicheza katika Kundi E.
Mechi ya fainali ya mashindano hayo itachezwa siku ya Jumapili mwaka huu.
Sports
Klabu ya Arsenal guu moja kuingia hatua ya Nusu fainali Klabu bingwa baada ya ushindi dhidi ya Sporting
Sports
Wakili George Kithi akabidhiwa rasmi Cheti cha uenyekiti wa bodi ya Michezo marufu kama Sports Arts and Social Development Fund (SASDF)
Waziri wa Wizara ya Masuala ya Vijana, Uchumi bunifu na Michezo, Salim Mvurya, ameshudia hafla rasmi ya kukabidhiwa uenyekiti wa Bodi ya Sports, Arts and Social Development Fund (SASDF) kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Jackson Tuwei kwenda kwa Mheshimiwa wakili George Kithi. Hafla hiyo ilifanyika, jijini Nairobi hii leo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri Mvurya alimpongeza Luteni Jenerali (Mstaafu) Tuwei kwa uongozi wake wa mfano na kujitolea kwake katika kipindi chake cha utumishi. Alibainisha kuwa chini ya uongozi wake, bodi hio iliimarika na kuwa taasisi imara na yenye mwitikio zaidi katika kusaidia na kuendeleza vipaji vya Wakenya.
Aidha, Waziri alieleza imani yake kwa uongozi wa Mheshimiwa wakili George Kithi, akimhakikishia ushirikiano na msaada kamili kutoka kwa Wizara katika kutekeleza majukumu ya Bodi kwa kipindi chake cha miaka mitatu.
SASDF inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kulea na kukuza vipaji vya Kenya, pamoja na kuimarisha hadhi ya nchi kimataifa kupitia michezo na uchumi wa ubunifu. Kupitia uwezeshaji wa wanamichezo, wasanii na wadau wa utamaduni, mfuko huo unachangia pakubwa katika ukuaji wa sekta za michezo na ubunifu nchini.

