News
Bunge la kitaifa kuhamasisha umma katika maonyesho ya Kilimo, Mombasa
Bunge la kitaifa linashiriki maonyesho ya kilimo ya kimataifa ya Mombasa kwa mara ya kwanza katika historia yake, ambayo yanaanza rasmi Jumatano Septemba 3, 2025 katika uwanja wa Mkomani.
Bunge hilo limeweka banda maalum la kuhamasisha umma kuhusu majukumu na shughuli zake.
Kamati ya kikosi kazi cha bunge inayoongozwa na mwenyekiti Owino Harrison ilishinikiza wananchi kujitokeza na kujifunza kuhusu historia ya bunge, utungaji sheria na nafasi ya taasisi hiyo katika utawala wa taifa.
Owino alisema uelewa wa umma kuhusu shughuli za bunge, una umuhimu mkubwa kwa kuwa bunge ni muhimili mkuu unaowakilisha sauti ya wananchi katika maamuzi ya kitaifa.
“Sababu kuu ya sisi kuja hapa ni kuwa tunataka kudhibiti wanafunzi kuja Nairobi kuja kujionea kinaechoendelea bungeni, watakapofika hapa watajionea kinachendelea kule, tunapanga kupeleka huduma zetu katika maonyesho mengine katika kaunti nyingine, pia tunafanya hivi kupitia hafla nyengine kama kongamano la ugatuzi”, alisema Owino
Kwa upande wake Mwenyekiti wa maonyesho hayo Henry Nyagah, aliedokeza kuwa maonyesho ya mwaka huu yanaangazia kilimo biashara akisistiza umuhimu wa vijana kushiriki katika hafla hiyo inayoambatanishwa na matumizi ya teknolojia na mabadiliko ya tabia nchi.
Zaidi ya washirika 200 wanahudhuria maonyesho hayo ambayo pia yamevutia washirika saba kutoka mataifa ya nje.
Maonyesho hayo yanakamilika Jumapili Septemba 7, 2025.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

