News
Mahafala baharini wahitimu kwa ujuzi mbalimbali
Kiwango cha mashindano ya kila mwaka ya mbio za jahazi ambayo huandaliwa katika mkono wa bahari wa Old Ferry mjini Kilifi, sasa kitapanda hadhi na kuwa tukio la kimataifa kitakachowaleta washiriki kutoka kote duniani na kukifanya kuwa kivutio cha kitamaduni na baharini kinachovuka mipaka ya taifa.
Mwenyekiti wa bodi ya Hazina ya ustawi wa michezo na sanaa Wakili George Kithi ambaye pia ni mgombea wa kiti cha Useneta kaunti ya Kilifi, alisisitiza dhamira ya kupiga jeki mashandano hayo.
Akizungumza katika hafla ya kipekee ya kuwakabidhi vyeti vya kuhitimu mahafala 68, baada ya kukamilisha mafunzo ya wiki mbili kuhusu mbinu za kuishi baharini, uokoaji majini na upigaji mbizi wa (scuba diving), Wakili Kithi alitaja kuwa mafunzo haya yamewapa vijana ujuzi wa kukabiliana na hatari majini, kutoa huduma ya kwanza, kujitetea na mbinu za ubaharia.

Mgombea wa nafasi ya useneti kaunti ya Kilifi Wakili Geroge Kithi, akizungumza na jamii ya sekta ya uvuvi katika eneo la Old Ferry mjini Kilifi
Aidha Wakili Kithi alisisitiza dhamira yake ya kuinua miradi ya Kilifi hadi viwango vya kimataifa kupitia hazina ya Michezo, Sanaa na Maendeleo ya Kijamii.
Mafunzo haya yenye manufaa makubwa yaliendeshwa na Shirika la Coast Sea Survival kwa ushirikiano na Kikosi cha Masuala ya Kiraia cha Jeshi la Wanamaji la Marekani, yakilenga kuwapa vijana stadi muhimu za kuokoa maisha na kujiendeleza katika sekta ya baharini.
Kithi alisema kwamba kupitia ruwaza yake atahakikisha bahari sio tu chanzo cha riziki bali pia ni daraja la matumaini na fursa mpya kwa vijana wa pwani.
Taarifa ya Lolani Kalu
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

