News
Murkomen, awataka machifu na polisi kupambana na pombe haramu
Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amewataka machifu na manaibu wao kuongeza juhudi katika vita dhidi ya pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya.
Waziri Murkomen alisema kuwa biashara na matumizi ya pombe haramu pamoja na dawa za kulevya vinaendelea kudhoofisha afya ya umma, usalama na utulivu wa kijamii nchini.
Akizungumza katika eneo la Cherangany kaunti ya Trans Nzoia, Murkomen alisema kuwa mapambano dhidi ya pombe haramu na mihadarati yanahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya serikali ya kitaifa, kanisa na jamii kwa ujumla.
“Tuko na jukumu kama serikali ya kitaifa kuhakikisha tunakomesha uuzaji wa pombe haramu na mihadarati kwa ushirikiano wa pamoja na makanisa na jamii kwa sababu hii biashara inafanyika sana mashinani na sasa ndio tunasema ni lazima tukomeshe hii biashara kabisa”, alisema Waziri Murkomen.

Waziri Murkomen katika kikao cha kiusalama na machifu na maafisa wa usalama
Aidha alisisitiza kuwa wasimamizi wa ngazi ya mashinani wana jukumu muhimu katika kusimamia sheria na kulinda jamii dhidi ya madhara ya bidhaa hizo haramu.
Waziri huyo alibainisha kuwa kaunti ya Trans Nzoia ni miongoni mwa kaunti zinazoongoza kwa visa vya pombe haramu na matumizi ya dawa za kulevya, hali aliyosema haikubaliki kamwe.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

