News
Mzozo kuhusu mradi wa unyunyizaji maji wa Bura waanza upya
Mradi wa unyunyizaji maji wa Bura katika kaunti ya Tanariver umeanza kushuhudia mvutano kuhusu umiliki wa ardhi.
Hii ni baada ya wakaazi wa eneo hilo kuitaka Mamlaka ya unyunyizaji maji NIA kutatua kwanza umiliki wa ardhi ya mradi huo sawa na kuweka wazi ekari za ardhi inazotumiwa kwa uendelezaji wa mradi huo wa unyunyizaji maji mashamba.
Wakaazi hao wanasema tangu mradi huo uanzishwe kumekuwa na mvutano kati ya wenyeji na mamlaka ya NIA kwani hata mipaka ya kuonyesha ardhi zinazotumika na Mamlaka hiyo imekosa kufichuliwa.
Wakaazi hao wamelalamikia kuwepo kwa njama ya kunyakuliwa kwa ardhi zao kwani serikali kuu kupitia Tume ya kitaifa ya ardhi imekosa kutoa hati miliki za ardhi kwa wakaazi wengi wa eneo hilo, hali ambayo wakihofikia kunyakuliwa kwa ardhi zao.
Wakizungumza katika kikao cha umma, wakaazi hao wamesema japo hawapingi uekezaji wa miradi ya umma ambayo itawasaidia pakubwa kujiendeleza kimaendeleo itakuwa bora zaidi iwapo mpango huo mwafaka utawekwa wazi kwa wananchi kwani ardhi inayotumika kwa mradi huo sio ya Mamlaka ya NIA.
Akizungumzia utata huo, mbunge wa Bura Yakub Adow, amelalamikia kutohusishwa na Mamlaka hiyo kuhusu ekari za ardhi ambazo zitatumika na Mamlaka hiyo, akisema kuna njama ya wananchi kunyanyaswa ardhi yao.
“Ukiangalia kwenye ramana ya ardhi utabaini kwamba ardhi hiyo ni zaidi ya ekari 170, lakini tukiwauliza mipaka ya ardhi hiii hawasema na hapo ndio inaleta shika kwa sababu wananchi wajua hii ardhi ni yao na NIA pia inatuambia kama ardhi pia ni yao, iko hadhibiti nyingi hatuelewi”, alisema Adow.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

