News
Ofisi ya DPP yafungua kesi ya nne dhidi ya Mackenzie
Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma, DPP, amefunga rasmi kesi ya nne na ya mwisho inayohusiana na mauaji ya halaiki ya watu katika msitu wa Shakahola, ambapo Mhubiri tata Paul Mackenzie na washtakiwa wengine 94 wanakabiliwa na mashtaka 238 ya kuua bila kukusudia.
Hatua hiyo imekuja baada ya shahidi wa 95 wa upande wa mashtaka ambaye ni mkuu wa upelelezi wa mauaji, Inspecta mkuu Raphael Wanjohi kuieleza Mahakama namna mtuhumiwa mkuu alivyodhibiti wafuasi wake hadi kusababisha vifo vya watu 429.
Akitoa ushahidi mbele ya Hakimu Mkuu Alex Ithuku, Wanjohi alisema Mackenzie na wenzake walikuwa na makubaliano ya pamoja ya kile alichokiita “mkataba wa kujiua,” wakidai kuwa walihamasisha kufunga hadi kufa kwa kisingizio cha kukutana na Yesu kabla ya mwisho wa Desemba 2020.
Aidha alieleza kuwa washtakiwa walikuwa na nia ya pamoja ya kusimamia vifo vya watoto na watu wazima kupitia mfungo wa kulazimishwa, huku wakijua wazi kuwa walikuwa wakitekeleza kitendo kisicho halali, jambo linalodhihirishwa na namna walivyoficha makaburi.
Upelelezi ulibaini kuwa Mackenzie alikuwa na kundi la ulinzi lililodhibiti mienendo ya watu na kuhakikisha mfungo huo unatekelezwa kikamilifu, huku mawasiliano ya simu yakionyesha ushirikiano wa karibu kati yake na wasaidizi wake.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

