Connect with us

News

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Pwani wanataka uwazi kuhusu kifo cha Ojwang’ 

Published

on

Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha pwani mjini Kilifi kaunti ya Kilifi walijitokeza na kuilaumu serikali wakidai kwamba imezembea kulinda usalama wa raia wake kutokana na visa vya mauaji ya mara kwa mara dhidi ya raia.

Wakizungumza nje ya lango la chuo hicho wakiongozwa na Vincent Obondo wanafunzi hao waliitaka serikali kuwachukulia hatua maafisa wote wanaohusishwa na kifo cha Albert Ojwang’ mwanablogu ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Obondo pia alilaumu viongozi wa kisiasa nchini ambao wameonekana kunyamazia kisa hicho cha mauaji ya Ojwang wakisisitiza kujiuzulu kwa Naibu Inspekta Jenerali wa polisi Eliud Laga’t ili kupisha uchunguzi.

“Albert hakujigongesha kwa ukuta jinsi ambavyo polisi wenyewe wanasema, sasa tunauliza serikali ni nini ambayo vijana walifanya ambacho kinakufanya uwachukie hivi, kwa viongozi wetu kwa nini mmenyamaza sana hamjajitokeza waziwazi kuuliza serikali kwa nini wanafanya, tuko hapa kuuliza na kuagiza serikali kuchukua hatua kwa Eliud Laga’t aweze kujiuzulu pamoja na msemaji wa huduma ya kitaifa ya polisi”, walisema wanafunzi hao.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Pwani wakilalamikia mauaji ya Albert Ojwang’

Walidai lalama zote zinaelekezwa kwa Naibu Inspekta jenerali wa polisi Eliud Laga’t hivyo anapaswa kuwajibishwa wakidai hakuna uhuru wa kujieleza nchini na serikali imekuwa ikiendekeza udikteta na kunyamazisha wakosoaji wake.

“Hata hiyo nafasi heri ibaki wazi kuliko yule jamaa awe pale, kwa sababu nchi yetu haiwezi kuwa namna hii, sisi vijana tutajitokeza namna gani kuonyesha tuko salama au hatuko salama, Nasimama hapa nikiwa na wasiwasi sana kwa sababu sijui nitakujiwa lini lakini hatuogopi na ikifika mwaka 2027 tunaambia kila mtu kuwa unakuja kwa kituo cha kupigia kura na vitu viwili, kwanza kitambulisho cha kitaifa na pili akili yako timamu”, waliongeza wanafunzi hao.

Kwa upande wao Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu kaunti ya Kilifi wakiongozwa  na Mwanase Ahmed, wameitaka serikali kuhakikisha maafisa wote wa polisi wanaohusishwa na visa vya mauaji ya raia kuwajibishwa.

“Sio mara ya kwanza kwa polisi kua wananchi hii kitu inaendelea na hakuna mtu ambaye amekamatwa na kufunguliwa mashtaka tangu mwaka jana, mimi nataka wachukuliwe hatua, tuko na jela, huu ni uhalifu dhidi ya binadamu”, aliongeza Mwanase.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.

Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.

Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.

“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.

Continue Reading

News

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma

Published

on

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.

Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.

Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.

Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.

“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi

Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Trending