Connect with us

News

Catherine Kenga ndiye spika mpya wa bunge kaunti ya Kilifi

Published

on

Catherine Kenga amechaguliwa kuwa spika wa bunge la kaunti ya Kilifi katika kikao maalum ambacho kiliandaliwa katika bunge hilo Jumatu Julai 21 2025.

Katika kikao hicho kilichoongozwa na naibu spika wa bunge hilo Naftal Kombo kwenye majengo ya bunge hilo mjini Malindi, Catherine Kenga alipata jumla ya kura 41, akifuatwa na wakili Faith Zawadi Kingi aliyepata kura 6 huku kura moja ikiharibika.

Wawakilishi wadi watatu walikosa kuhudhuria kikao hicho ingawa sababu za viongozi hao kukosa  kuhudhuria hazikuwekwa bayana.

Kenga anachukua hatamu ya kuliongoza bunge hilo kutoka kwa aliyekuwa spika Teddy Mwambire ambaye alitimuliwa  mapema mwezi uliopita Juni 30, 2025 kupitia kura ya maoni.

Mwambire alibanduliwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na ukiukaji wa katiba.

Catherine  ni miongoni mwa wagombeaji wanne waliotuma maombi ya kuwania wadhifa huo baada ya kujiuzulu kama waziri wa barabara katika serikali ya Kaunti ya Kilifi chini ya uongozi wa gavana Mung’aro.

Pichani:Kutoka kushoto,Karani wa bunge la kaunti ya Kilifi, Micheal Ngala, gavana Gedion Maitha Mung’aro na spika wa Sasa Catherine Kenga (Picha Kwa hisani

Catherine Kenga atakuwa spika wa tatu kulihudumia bunge hili, baada ya spika wa kwanza Jimmy Kahindi ambaye alihudumu kwa vipindi viwili chini ya uongozi wa gavana Amason Kingi ,ambaye sasa ni spika wa bunge la seneti.

Teddy Mwambire ndio alichukua wadhifa huo baada ya uchaguzi mkuu wa 2022, aliposhindwa na Kenneth Kazungu  Charo almaarufu ‘Tungule’ katika kinyang’anyiro  cha ubunge  wa  Ganze.

Catherine Kenga sasa anajukumu la kuleta mshikmano katika bunge hilo linalokabiliwa na mgawanyiko  kati ya wandani wa gavana Mung’aro kwa upande mmoja na wale ambao walimuunga mkono Teddy Mwambire wakati kura ya kutokuwa na imani naye ilipopigwa.

Kuwepo kwa maafisa wa ngazi za juu kutoka  serikali ya gavana Mungaro wakati wa kura hiyo ni ishara ya wazi kwamba spika wa sasa Catherine Kenga ana usuhuba na serikali ya sasa ya  gavana Mung’aro.

Hata hivyo, kura hiyo ilipigwa licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama lililotolewa  wiki mbili zilizopita  kusitisha mipango ya kumtimua Teddy Mwambire hadi kesi iliyowasilishwa mahakamani kusikilizwa na kuamuliwa.

Miongoni mwa walioshiriki kura hiyo ni pamoja na Tendai Mtana Lewa, na Mazera Shadrack.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.

Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.

Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.

“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.

Continue Reading

News

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma

Published

on

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.

Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.

Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.

Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.

“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi

Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Trending