News
EPRA yatangaza ongezeko la bei ya mafuta
Madereva nchini sasa watalazimika kulipa zaidi kwa mafuta baada ya Mamlaka ya kudhibiti bei ya Petroli nchini EPRA kutangaza ongezeko la bei za mafuta kwa kipindi cha Mei 15 hadi Juni 14, 2026.
Katika mabadiliko mapya yaliyotangazwa usiku wa kuamkia leo, EPRA imeeleza kuwa gharama ya Super Petroli na Dizeli imeongezeka kwa shilingi 16.65 na shilingi 46.29 kwa lita.
Jijini Nairobi, Super Petroli, Dizeli na mafuta ya taa sasa itauzwa kwa shilingi 214.25, shilingi 242.92 na shilingi 152.78 mtawalia kwa siku 30 zijazo.
Jijini Mombasa, Super Petroli, Dizeli na mafuta ya taa sasa zitauzwa kwa shilingi 211.09, shilingi 239.64 na shilingi 149.49 mtawalia.
EPRA imesema kuwa marekebisho hayo yanaakisi kupanda kwa bei za bidhaa za petroli katika soko la kimataifa, pamoja na mabadiliko ya kiwango cha ubadilishaji wa fedha na utekelezaji wa ushuru wa kisheria, chini ya mfumo wa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Kulingana na EPRA, Serikali itawasaidia watumiaji kupitia Mfuko wa ushuru wa maendeleo ya petroli (PDL) kwa kutumia takriban shilingi bilioni 5, kufadhili bei za Dizeli na mafuta ya taa.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

