News
Idara ya hali ya hewa nchini yaonya kuhusu mvua mkubwa
Idara ya hali ya hewa nchini imeonya kuwa mvua za wastani hadi mvua nyingi zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya Nairobi na kaunti jirani katika saa 24 zijazo.
Katika taarifa yake idara hiyo imesema mvua hizo zitaathiri hasa maeneo ya nyanda za juu mashariki mwa Bonde la Ufa, ikiwemo Kaunti ya Nairobi.
Kulingana na utabiri huo, hali ya mawingu inatarajiwa asubuhi ya leo kabla ya kupisha vipindi vya jua, huku kukiwa na uwezekano wa mvua nyepesi katika maeneo ya nyanda za juu.
Kaunti za pwani, zikiwemo kaunti ya Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamuna Tana River, zinatarajiwa kupata manyunyu mepesi ya mvua, huku mvua zaidi zikitarajiwa asubuhi ya leo na alasiri, hasa katika pwani ya kusini.
Utabiri huo pia umeonya kuhusu upepo mkali wa kusini mashariki unaozidi mafundo 25katika baadhi ya maeneo ya Kaunti ya Turkana na Kaunti ya Marsabit.
Taarifa ya Joseph Jira
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

