Connect with us

News

Mahakama Kuu yasitisha mpango wa Marekani na Kenya wa Karantini

Published

on

Mahakama Kuu nchini imesitisha kwa muda mpango wa serikali ya Marekani na Kenya wa kuanzisha kituo cha karantini cha Ebola humu nchini.

Jaji wa Mahakama hiyo, Patricia Nyaundi, ameagiza kusitishwa kwa muda kwa utekelezaji wa makubaliano hayo hadi pale kesi iliyowasilishwa Mahakamani itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Katika uamuzi wake, Jaji Nyaundi alisema Kenya pia hairuhusiwi kupokea mtu yeyote aliyekumbana na Ebola au aliyeambukizwa ugonjwa huo chini ya mpango huo hadi kesi hiyo itakapomalizika.

Shirika la kutetea haki za kiraia la Katiba Institute liliwasilisha kesi hiyo mahakamani likipinga mpango huo siku hiyo hiyo ulipotangazwa.

Shirika hilo limesema kuanzishwa kwa kituo hicho kwa siri na bila ushirikishwaji wa umma kunazua maswali mengi kuhusu haki za maisha, afya, uwajibikaji wa serikali na usimamizi wa bunge.

Kabla ya kesi hiyo kuwasilishwa Mahakamani, Serikali ya Marekani kupitia Rais Donald Trump ilikuwa imekubaliana na Kenya na kutangaza mpango wa kuwahifadhi kwa muda raia wake waliokumbana na virusi vya Ebola nchini Kenya.

Hatua hii ililenga kuzuia ugonjwa huo kuingia katika ardhi ya Marekani, ambapo sasa mpango huo umekumbana na kikwazo kikubwa baada ya Mahakama kuu nchini kusimamisha kwa muda mpango huo.

Kwa mujibu wa Ikulu ya White House, raia wa Marekani waliokuwa katika maeneo yenye mlipuko wa Ebola lakini hawajaonyesha dalili za ugonjwa huo walitarajiwa kuwekwa katika kituo maalum cha karantini katika Kambi ya Anga ya Laikipia mjini Nanyuki.

Maafisa wa utawala wa Marekani walikuwa wamesema wale ambao wangepata dalili za Ebola hawangerejeshwa Marekani, bali wangepelekwa katika nchi nyingine kwa matibabu ya juu zaidi.

Hatua hiyo ilionekana kuwa mabadiliko makubwa ya sera ikilinganishwa na milipuko ya Ebola iliyopita ambapo wagonjwa Wamarekani waliruhusiwa kurejeshwa nyumbani kwa matibabu.

Lengo la mpango huo lilikuwa kuhakikisha hakuna kisa cha Ebola kinachoingia nchini Marekani.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Aisha Jumwa akihama rasmi chama cha UDA

Published

on

By

Mgombea wa kiti cha ugavana wa kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa amekihama rasmi chama cha UDA, akisema atatangaza baadaye mwelekeo atakaochukua wa kisiasa.

Jumwa alitoa tangazo hilo katika kikao na Wanahabari kilichofanyika katika makaazi yake, eneo la Kakuyuni huko Malindi kaunti ya Kilifi leo siku ya Alhamis.

Hatua ya Jumwa ilijiri baada ya kuwepo na tetesi kwamba alikuwa na mipango ya kuhama chama hicho kutokana na sintofahamu za kisiasa ndani ya chama cha UDA kuhusu msimamo wake wa kisiasa wa kuwania nafasi ya ugavana wa Kilifi.

Jumwa alilalamika kwamba alikuwa akinyanyaswa na baadhi ya viongozi hata kutimuliwa katika Ikulu ya rais licha ya kupambana katika kampeni za rais Ruto mwaka wa 2022, akionekana kumlaumu rais Ruto kwa kutomjali tena hata baada ya kusimama na yeye kisiasa.

Kiongozi huyo alikashfu vikali kutengwa katika mikutano ya UDA licha ya kuwa mwandani wa rais Ruto na pamoja na kufanyikisha miradi ya serikali mashinani, akisema tangu atangaze mchakato wa kuwania kiti cha ugavana wa Kilifi mwaka wa 2027, amekuwa akipitia masaibu mengi.

Hii sio mara ya kwanza kwa Jumwa kukihama Chama cha UDA na kurejea kwenye chama hicho, lakini hatua aliyoichukua sasa itabadili masimamo wa kisiasa kaunti ya Kilifi.

Itakumbukwa kwamba Jumwa amekuwa mwandani wa karibu wa rais William Ruto, lakini hatua aliyoichukua huenda ikabadili msimamo wa kisiasa kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla. 

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

News

Mahakama ya Kilifi yaagiza kuzuiliwa Washukiwa 7 wa mauaji

Published

on

By

Mahakama ya Kilifi imeagiza kuzuiliwa kwa siku 14 washukiwa 7 wanaotuhmiwa kuhusika katika kifo cha mwanamke mmoja aliyekuwa na umri wa miaka 65, ambaye aliuwawa kwa tuhma za uchawi katika eneo la Malomani eneo bunge la Ganze kaunti ya Kilifi.

Washukiwa hao Gilbert Karisa Changawa, Selvestar Changawa Kahindi, Elizabeth Jackson Ngala, Dhahabu Kithi Kombe, Dzendere Palu Kalama, Agness Changawa na Kadzo Ngombo Bienge watazuiliwa katika kituo cha Bamba wakati uchunguzi ukiendelea.

Kulingana na Afisa mpelelezi kutoka kitengo cha DCI ameeleza mahakama kwamba ilikuwa mnamo tarehe 27 mwezi huu ambapo walipokea tarifa kwamba dama changawa alikuwa amekatwa kichwa na kuuwawa na watu wasiojulikana usiku huo.

Afisa mpelelezi pia ameeleza kuwa washukiwa ambao ni wanafamilia,siku kabla ya tukio husika walikuwa wameandaa kikao cha kudumisha Amani baada ya kifo kilichokuwa kimetokea kwa kijana mmoja mtoto wa mmoja kati ya washukiwa aliyefariki kaunti ya Mombasa baada ya kupigwa kwa tuhma za wizi.

Kutokana na kifo cha kijana huyo wanafamilia hao walimtuhmu dama kwamba ndiye aliyekuwa amemroga kijana huyo na kusababisha kifo hicho cha gafla, ambapo usiku huo Dama aliuwawa nyumbani kwake.

Washukiwa watarudishwa mahakamani tarehe 13 mwezi Agosti mwaka huu baada ya uchunguzi kukamilika.

Taarifa ya Teclar Yeri

Continue Reading

Trending