Connect with us

News

Ujenzi wa barabara ya Kibaoni-Ganze-Bamba umeng’oa nanga

Published

on

Baada ya wakaazi wa eneo bunge la Kilifi Kaskazini na Ganze kulalamikia ubovu wa barabara ya Kibaoni-Ganze hadi Bamba na kuangziwa na wanahabari, hali sasa ni tofauti.

Ujenzi wa barabara hiyo iliyoshudia utata na maandamano, sasa unaendelea huku mkandarasi akiwa katika hatua kupiga msasa barabara na kujenga mabomba na sehemu za kupitisha maji hasa kunaponyesha.

Justine Kandie ni muangalizi wa ujenzi wa barabara hiyo, alisema shughuli hiyo imegawanywa mara mbili, na kwa sasa wameanza ujenzi wa barabara hiyo kutoka eneo la Kibaoni mjini Kilifi kuelekea Ganze.

Kandie alisema mpango huo ulianza mwaka 2021 kutoka eneo bunge la Ganze kuelekea kibaoni japo ulisitishwa wakati huo na sasa wameanza tena kujenga umbali wa kilomita tano.

“Katika awamu ya kwanza kwa mwaka wa 2021 tulianza barabara kutoka Ganze tulikuwa tunafanya kilomita tano, kwa mda wa miaka miwili barabara ikasimama kidogo, baadaye kurudi kwa huu mwaka wa 2025 ndio tumepewa kile kiwango tuanze kutoka kibaoni kuelekea Ganze, katika hii awamu ya pili tunafanya kilomita tano ila kwa sababu barabara ni mbovu tumeamua kuanzia huku kwa Kimanje tukielekea Kibaoni ili barabara yetu iwe sawa wakati tunaposafirisha vifaa vya ujenzi”,alisema Kandie.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya kuelekea Ganze

Picha:(Joseph Jira)

Kandie pia alisema mda wa miaka miwili aliopewa mkandarasi kukamilisha ujenzi huo wa barabara utategemea na mgao wa pesa zitatakaotolewa kufanikisha mradi huo.

“Ule mda wa kukamilisha barabara huwa inategemea uwezo wa mwanakandarasi kama ako na fedha za kutosha, itamsaidia kukamilisha kwa mda unaofaa, kwa sababu hii barabara yetu walikuwa wametupa kama miaka miwili ila saa hii mda umesonga”, aliongeza Kandie.

Wakaazi pamoja na wahudumu wa uchukuzi wa umma wanaotumia barabara hiyo wameeleza matumaini ya kuimarika kwa sekta ya uchukuzi sawa na uchumi mara tu ujenzi utakapokamilika.

Itakumbukwa kwamba barabara hiyo ilileta utata na kusababisha wakaazi kuandamana na kuifunga sawa na kutatiza shughuli za usafiri kwa mda.

 “Hapo kwa usafiri na biashara huenda kukabadilika kwa sababu wengi pia wanakataa huku kwa sababu yah ii barabara vile ni mbovu hasa kazi zinakuwa ziko chini kwa sababu ya vumbi”,alisema Jeremiah Mwaringa

Tinga tinga za ujenzi wa barabara ya kuelekea Ganze.

Picha:(Joseph Jira)

Mvutano huo pia ulishuhudiwa baina ya mbunge wa Ganze Kenneth Kazungu Tungule na mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya kuhusu ujenzi wa barabara unakofaa kuanza kutekelezwa.

Hata hivyo muangalizi wa mradi huu aelieleza matumaini yake kuwa mvutano huo wa wanasiasa hautaathiri utendakazi wao huku akishinikiza wahudumu wa barabara hiyo kuwa na uvumilivu wakati wanapoendelea na ujenzi huo.

Taarifa ya Joseph Jira

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.

Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.

Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.

“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.

Continue Reading

News

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma

Published

on

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.

Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.

Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.

Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.

“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi

Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Trending