News
DCI yaruhusiwa kufukua makaburi Kwa Binzaro Kilifi
Idara ya upelelezi wa jinai DCI imepewa ruhusa na mahakama ya Malindi, kuanza kufukua makaburi yaliyotambuliwa katika kijiji cha Kwa Bi Nzaro kilomita sita kutoka eneo la Shakahola eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.
Hii ni baada ya makaburi zaidi kugunduliwa katika eneo hilo lenye msitu na kuzua taharuki miongoni mwa wakaazi, huku ikihofiwa kuwa huenda wafuasi zaidi wa dhehebu potovu katika eneo hilo wamefariki.
Wizara ya usalama nchini ilisema imetibua kuenea kwa dhehebu hilo ambalo linakisiwa kuandamana na mafunzo ya itikadi kali kama ilivyoshuhudiwa katika msitu wa Shakahola miaka miwili iliyopita.
Oparesheni ya polisi ilifichua boma lililoko kwenye ardhi ya ekari tano linaloaminika kutumika kuwahifadhi wafuasia wa dhehebu potovu.
Wakaazi katika kijiji hicho walihofia huenda kunamiili mingine ambayo imezikwa katika sehemu hiyo ya ardhi baada ya mwili na mafuvu ya kichwa kupatikana maeneo hayo.
Mshukiwa mkuu anayedaiwa kuendeleza imani hio ni jamaa mmoja aliyeokolewa kutoka Shakahola nakurejeshwa kwa familia yake kaunti ya Siaya kabla ya kurejea Kilifi mapema mwaka wa 2025.
Alikamatwa pamoja na wengine na kufunguliwa mashtaka mahakamani Malindi kaunti ya Kilifi.
Taarifa ya Joseph Jira.
News
Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA
Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane
Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.
Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.
Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.
“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.
News
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma
Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.
Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.
Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.
Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.
“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi
Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

