Connect with us

News

Gavana Lusaka afutilia mbali baraza lake la mawaziri

Published

on

Gavana wa kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka, amefutilia mbali baraza lake la mawaziri akilenga kulifanyia mabadiliko ili kuimarisha utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo.

Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya bahari na kutiwa saini na Gavana huyo, imebaini kwamba Katibu wa kaunti pamoja na Mwanasheria mkuu wa kaunti pia wamesimamishwa kazi, hatua hii ikitekelezwa miezi michache tu kabla ya uchaguzi mkuu ujao mwaka wa 2027.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na serikali ya kaunti hiyo, Gavana Lusaka alieleza kwamba hatua hiyo imetokana na utendakazi duni wa viongozi hao pamoja na kutofikia malengo ya wananchi kwa kuambatana na ajenda za Gavana huyo.

Gavana Lusaka alisema kwa kuzingatia kipengele cha 40 ibara ya kwanza sehemu ya {a}, ambayo inampa mamlaka ya kuwasimamisha kazi maafisa wakuu wa kaunti pamoja na kulivunja baraza la mawaziri, Gavana Lusaka alichukua hatua hiyo ili kuimarisha utendakazi wa kaunti.

Taarifa ya kusimamishwa kazi kwa baraza la mawaziri iliyotolewa na Gavana wa Bungoma Kenneth Lusaka

Taarifa hiyo pia ilifafanua kwamba ilichukuliwa kwa nia njema na kwa maslahi mapana ya umma, ikiongeza kwamba inalenga kuwezesha utendaji bora ndani ya utawala wa kaunti pamoja na kulinda uadilifu wa taasisi za umma.

“Nataka kuwahakikisha wakaazi wa kaunti ya Bungoma kwamba mabadiliko hayo makubwa hayataathiri huduma za kaunti kwani ni hatua moja wapo ya kuboresha utendakazi wa kaunti hiyo”, alisema Gavana.

Aidha alieleza kwamba mawasiliano zaidi kuhusu mipango ya muda na uteuzi mpya yatatolewa baadaye, kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Hata hivyo tetesi kutoka kwa wandani wa kisiasa, walisema kwamba hatua hiyo imechochewa kisiasa ili kuzuia mchakato uliyokuwa umepangwa wa kuwasilisha hoja bungeni ya kuwabandua uongozi baadhi ya mawaziri wa serikali ya kaunti hiyo kutokana na utendakazi duni na ufisadi.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.

Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.

Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.

“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.

Continue Reading

News

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma

Published

on

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.

Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.

Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.

Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.

“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi

Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Trending