Connect with us

News

Polisi wanasa magunia 12 ya bangi Malindi

Published

on

Maafisa wa kukabiliana na dawa za kulevya Malindi katika kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na maafisa wa kitengo maalum cha oparesheni SOG kilicho katika kizuizi cha polisi daraja la Sabaki, wamekamata gari aina ya Toyota SUV likiwa limejaa dawa za kulevya aina ya bangi.

Maafisa hao walisema walikuwa na taarifa muhimu kuhusu gari hilo lililokuwa likisafirisha mzigo huo haramu ambapo waliweka mtego wa kusimamisha gari hilo katika eneo la Gede ila dereva alikaidi amri ya kusimama.

Ilisemekana badala yake aliongeza mwendo akigeukia barabara ya Jacaranda kutoka Kijiwetanga katika jaribio la kutoroka.

Msako mkali uliendeshwa na baada ya saa chache gari hilo lilipatikana likiwa limeachwa eneo la Mayungu nambari zake za usajili zikiwa zimebadilishwa haraka katika harakati za kuwapotosha maafisa wa upelelezi.

Baada ya ukaguzi maafisa walibaini kuwa gari hilo lilikuwa na magunia 12 ya bangi, mzigo unaokisiwa kuwa na thamani ya mamilioni ya pesa, na ambao ulikuwa ukielekezwa mitaani.

Taarifa ya Joseph Jira 

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

News

Kaunti ya Kilifi yatenga shilingi milioni 10 kusimamia wajane kwa SHA

Published

on

By

Serikali ya kaunti ya Kilifi imedai kwamba imetenga shilingi milioni 10 kusimamia huduma za afya kwa wajane

Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro aliwataka wajane na wanawake ambao bado hawajajisajili katika SHA, kutumia fursa hiyo ili iwe rahisi kwao kupata huduma za matibabu hospitalini.

Mung’aro aliwataka Wanawake wa kaunti ya Kilifi kuanza mchakato wa kuwasajali wajane katika SHA, akisema serikali ya kaunti iko na mipango ya kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma za matibabu bila changamoto.

Kiongozi hiyo pia alisema mikakati mwafaka imeidhinishwa kuhakikisha changamoto za urithi wa mashamba kwa akina wajane inashughulikiwa kupitia mawakili wa serikali ya kaunti.

“Naibu wangu ni mama, tuko na maafisa watano ni mama, kwa hivyo ni wajapange washirikiane na mawakili wa kaunti ili kupata haki ya urithi na tumetenga shilingi milioni 10 kusaidia wajane kujiandikisha na SHA ili wapate huduma za matibabu bila changamoto”,alisema Mung’aro.

Continue Reading

News

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki kwa umma

Published

on

Serikali imepiga marufuku uagizaji wa dawa za Antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda katika makaazi ya umma, ikisema mwenendo huo hautakubalika.

Waziri wa Afya nchini Adan Duele amesema serikali kupitia Wizara ya Afya nchini na Bodi ya dawa na sumu nchini zimeweka mikakati mwafaka ya kulinda afya ya wananchi.

Duale alisema wakenya hawafai kuilaumu bodi ya dawa na sumu nchini kutokana na sheria ngumu ilizotoa bali kuridhia hatua hiyo ili kuzuia madhara.

Akizungumza wakati wa warsha ya mikakati ya kuboresha afya ya umma, Waziri Duale alisema hatua hiyo inaanza kutekelezwa mara moja, huku akisisitiza kwamba serikali haitalegeza kambi katika kulinda afya ya umma.

“Kuanzia sasa hakuna tena kuagiza dawa za antibiotiki na kusafirishwa na wahudumu wa bodaboda kwani hatua hiyo ni hatari, wewe uko nyumbani kisha unaagiza dawa sini hiyo ni hatari, na hakuna kulaumu bodi ya dawa na sumu nchini kwa sababu tumeweka sheria hiyo”, alisema Duale.

Warsha ya watafiti wa kisayansi iliyiofanyika jijini Nairobi

Waziri huyo wa Afya nchini alishikilia kwamba hatua waliochukua mwafaka kwani italinda afya ya wananchi, akiwaonya wale wanaoendeleza bishara hiyo haramu. kusababisha madhara.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi

Continue Reading

Trending